![](http://api.ning.com/files/Ktsylelmf0kc8IARa5G7kBwkSNOYsq2c02DSaFIfA6xg3LggJevzI0xKBmENYP572MMxleo7VH4a*uLDY8bR1TW2-3*2HlKB/wemasepetu.jpg?width=650)
Wema Sepetu akitafakari jambo.
LILE
ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na
aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeanza kumchefua
mrembo huyo kiasi cha kulisusa.
![](http://api.ning.com/files/Ktsylelmf0l5GmXNaskUlxaSvujkUo5A7jX1E-011C9OFwhDc7Hfb*Z8X3XNp7SlkVzyK*R6e1*VumoLbmD6KJDxVAt1B9FK/murano111.jpg?width=650)
Ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond'.
Tukio
hilo lilijidhihirisha wazi mbele ya paparazi wetu juzikati nyumbani kwa
staa huyo, Kijitonyama jijini Dar, ambapo Wema alitamka hadharani kuwa
kwa sasa analichukia kupita maelezo gari hilo alilozawadiwa na Diamond
kwenye sherehe yake ya kuzaliwa.
“Bwana
acha nitumie hili gari lingine kwenda airport hilo Murano sitaki hata
kulisikia, sijui najisikiaje hata nikiliona,” alisikika Wema.Paparazi
wetu baada ya kusikia Wema akionesha wazi kuwa analichukia gari hilo,
alimuuliza sababu inayomfanya alichukie ambapo alisema hajui ni kwa nini
analichukia ingawa ni mali yake.
“Siku
hizi sipendi kutumia hili Murano tena nalichukia kweli, inafikia
kipindi nakosa raha nikiliona lakini ukiniuliza sababu ya kulichukia
kiasi hicho hata sina sijui nimezoea sana kutumia BMW, ndiyo maana
najikuta nalichukia gari hili,” alisema Wema.
![](http://api.ning.com/files/Ktsylelmf0kqgMvB-Kn*88tIJVFTaEY0iYcWhRmZBwKHr4FpxnnyjqwEGe718Wgvccl*FVhwShtZUuWsT-utoLqcI8j*rZ3y/diamondplatnumz.jpg?width=650)
Nasibu Abdul ‘Diamond'akipozi.
Kwenye
bethidei yake iliyofanyika Septemba, mwaka huu, Wema alizawadiwa magari
mawili. La kwanza lilikuwa ni BMW 545i (Sh. Milioni 56) ambalo liliibua
utata juu ya mtu aliyemzawadia na la pili ni Nissan Murano (Sh. milioni
36) alilopewa na Diamond.
إرسال تعليق