Msanii maarufu wa mjini Mombasa, Kenya, Susumila amekanusha
taarifa zilizotapaa mjini humo kuwa yeye na Nyota Ndogo walidhalilishwa
na Diamond pamoja na mwandaaji wa show yake iliyofanyika huko weekend
iliyopita.
Mtandao wa Standard Media wa Kenya,
uliandika kuwa kwenye show hiyo iliyohudhuriwa na watu kibao, Diamond
alitaka wasanii wengine wote waliokuwa watumbuize kwenye show hiyo na
waliokuwa wamepangiwa kukaa naye kwenye VIP lounge, wakiwemo Susumila na
Nyota Ndogo waondelewe.
Ilidaiwa pia kuwa Susumila na Nyota Ndogo walinyimwa maji ya kunywa
na kwamba waliambiwa wanywe maji ya bomba kwakuwa maji ya kwenye chupa
yalikuwa kwaajili ya Diamond peke yake na kwambatukio hilo liliwafanya
wasanii wa Mombasa waungane kuwalaani waandaji wa show hiyo ambapo VJ
Delph alikataa kucheza muziki.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto, Willy M Tuva wa
Radio Citizen leo, Susumila amedai kuwa hizo ni habari za uzushi.
Susumila
“Hizo story ni za uongo,” amesema msanii huyo. “Sidhani kama Diamond
anaweza kufanya hivyo au ana haki ya kufanya hivyo. Kama nimekuwa
mistreated labda niwe mistreated na yule mtu amenipatia show, sio
Diamond sababu naye ameitwa kwenye show kama mimi,” ameongeza.
“Unajua Mombasa wanapenda vitu vya uongo, hakuna mtu ana complain
kuhusu show ilikuwa mbovu ama nini, watu wanatafuta vijisababu vidogo
vidogo wanasema sijui nimenyimwa maji. Mimi nilipanda steji nilikuwa na
chupa yangu ipo kwa DJ, nikaperformm dancers wangu walipokuwa wameingia
wanafanya set yao nikachukua maji nikanywa pale pale kwa DJ kulikuwa na
chupa kama kumi za maji hazijafunguliwa. Sijui story ilianzia wapi
lakini kufikia kwenye saa tatu, saa nne ilikuwa kwenye blog karibu zote
za huku (Mombasa).”
Msikilize zaidi hapo chini
إرسال تعليق