HOSPITALI YA MISHENI YA SENGEREMA LAWAMANI KWA KUMUWEKEA DAMU ISIYO GROUP LAKE MTOTO WA MIAKA 5 NA KUSABABISHA KUPOOZA MWILI MZIMA
Hospitali
ya Misheni Wilayani Sengerema mkoani Mwanza imepata lawama kutokana na
kitendo chake cha kumuongezea damu ambayo siyo kundi lake
mtoto aliyeafahamika kwa jina la Salome Pastory mwenye umri wa miaka
mine.
Taarifa
hizo zimegundulika kufuatia baba wa mtoto huyo Edward Pastory kufika
katika ofisi za Kijukuu Blog zilizopo Mjini Kahama kwa lengo la kuomba
msaada wa kuwekwa mtandaoni ili apatiwe msaada.
Pastory
alisema kuwa mtoto wake alianza kuugua mafua na kichwa na alipoikishwa
katika hospitali ya mgodi wa Bulyanhulu iliyopo wilayani Kahama
aliambiwa mtoto wake ana upungufu wa damu na maji.
Kufuatia
majibu hayo Pastory akiwa na mke wake waliamliwa kwenda hospitali ya
misheni iliyopo Wilayani Sengerema ili awez kusaidiwa kuongezewa damu na
kupatiwa matibabu makubwa.
Inadaiwa
kuwa mtoto huyo ambaye alikuwa na damu ya Kundi 0 aliongezewa damu ya
kundi A Hali iliyopelekea kupooza viungo vyake vyoye vya mwili ikiwa ni
pamoja na kuacha kuona kabisa kwa miaka mitatu sasa.
Taaarifa
za mtoto huyo kuchanganyiwa damu zilitolewa na daktari ambaye
hakufahamika jina katika hospitali ya misheni ya Sengerema alipowaomba
radhi wana familia wa mtoto huyo kuwa walipitiwa na kujikuta wamefanya
kosa hilo na kuwaomba watafute damu ya kundi 0 ili wamuwekee tena mtoto
huyo.
Baada
ya tukio hilo mama wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Yulitha
Jeremiah aliamua kukimbia na kumtelekeza mtoto huyo kwa baba yake hali
iliyopelekea baba yake kumpeleka mwanaye kwa bibi yake Mereciana Malele
aishie katika kijiji cha Kishimba mkoani Geita.
Kwa
mujibu wa baba wa mtoto huyo baada ya kuona tatizo linakuwa sugu
aliamua kumpeleka mwanaye katika hospitali ya rufaa ya Bugando ambapo
aliambiwa atafute shilingi laki tano ili mtoto wake aweze kukaa,kusimama
na kushika vitu huku akiambiwa macho yake yataendelea kutoona.
Kufuatia
hali ya ukata ya baba huyo aliamua kufika ofisi za mkuu wa wilaya ya
Kahama na kuomba kuandikiwa barua maalumu ya kuomba msaada kwa wasalimia
wema.
Taarifa
zilizopatikana kufuatia barua hiyo hivi sasa Edward amefanikiwa
kukusanya kiasi cha shilingi laki moja na kwamba bado anahitaji laki nne
ili kuweza kumsaidia mwanaye.
Kutokana
na tatizo hilo Edward ameamua kuweka namba zake hapa 0764-769868 ili
kwa yeyote atakayeguswa jambo hili aweze kumsaidia na kumpigia ili ampe
habari kamili la tukio hili.
MATUKIO KATIKA PICHA:
BABA WA MTOTO HUYO KULIA AKIWA NA MTOTO WAKE.
AKICHEZA NA MTOTO WAKE
MWANDISHI NA MMILIKI WA KIJUKUU BLOG AKIWA AMEMBEBA MTOTO SALOME
HAPA AKIJARIBU KUMSIMAMISHA LAKINI ILIKUWA NGUMU SANA.
MTOTO SALOME AKIWA AMELALA HAWEZI KUKAA WALA KUSIMAMA..
إرسال تعليق