
Kwa
wale wazazi ambao ni wanajishughulisha na kazi mbalimbali hivyo
kujikuta wakilazimika kutafuta wasichana wa kazi ili wawasaidie majukumu
ya kubaki na watoto nyumbani, mshtuko mkubwa Duniani uliibuka huku kila
mzazi ambaye huwa anamuacha mtoto na msichana wa kazi nyumbani
kujiuliza juu ya usalama wa watoto wao kutokana na kitendo cha msichana
mmoja kumpiga na kumuumiza mtoto na ushahidi wa kitendo hicho kupatikana
kwenye kamera iliyotegeshwa bila yeye kujua.
Hiyo ilikuwa ni ya kutoka Uganda, kituo cha Citizen TV
cha Kenya kimeripoti tukio jingine linalofanana na hilo ambapo msichana
mmoja amefikishwa Mahakamani pia baada ya kurekodiwa na kamera akimpiga
mtoto mdogo wa miaka mitatu na kumuumiza.
Msichana huyo Janeth Muthoni Karanja
alikubali kufanya kosa hilo, kesi yake itaendelea siku ya Jumatano,
huku yule msichana wa Uganda kesi yake kuendelea kusikilizwa Jumatatu ya
wiki ijayo, Desemba 08.
Unaweza kuisikiliza hapa Ripoti ya taarifa hiyo ambayo nimekurekodia wakati ikirushwa hewani nakituo cha Citizen TV.
إرسال تعليق