Ikulu yaitisha mkutano na Wanahabari Jumatatu 22 Desemba saa Tatu Kamili Asubuhi

Taarifa iliyotolewa jana usiku  na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam, ilieleza kuwa kumeitishwa Mkutano na waandishi wa habari Jumatatu asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mkutano utafanyika leo saa tatu kamili asubuhi na kila chombo kimetakiwa kutuma Mwandishi pamoja na mpiga picha ambao wametakiwa kuwa tayari wameketi vitini ifikapo saa Mbili Unusu bila kuchelewa wala kukosa.

Agenda ya mkutano huo ni "SHUGHULI MAAUM"  na hakuna ufafanuzi zaidi uliotolewa.

Ikumbukwe pia kwamba leo mchana  Rais Kikwete ataongea na wazee wa Dar es salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post