![](http://www.itv.co.tz/media/image/dar14.jpg)
Jeshi
la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia kimelazimika kuingilia kati ili
kulinda usalama baada ya wananchi wa vingunguti kushindwa kupiga kura
katika uchaguzi wa serikali za mtaa kwenye kituo cha kata ya Mtambani
kutokana na Kukosekana kwa baadhi ya karatasi za kupigia kura.
ITV imefika katika kituo hicho kilichopo katika ofisi ya afisa
mtendaji kata ya Mtambani na kukuta mamia ya wananchi wakihamasishana
kwa nyimbo mbalimbali huku, huku mmoja wa wananchi hao akishilikiwa na
jeshi la Polisi kutokana na kukutwa na karatasi za kupigia kura ambapo
askari wa jeshi la Polisi wengine wakiwa juu ya magari yao na wengine
wakizuia watu kuingia ndani ya kituo hicho.
Wakizungumza na ITV baadhi ya wananchi hao licha ya kupinga zoezi
la kupiga kura kuhamishiwa siku ya jumamosi wameilalamikia serikali kwa
kushindwa kuwa na mifumo mizuri ambayo ingewezesha upatikanaji wa
karatasi za kupigia Kura kulingana na idadi ya watu walijitokeza
kujiandisha kwa wiki moja.
Hali ya kuahirishwa kwa uchagzu wa serikali za mitaa imejitokeza
pia katika kata ya Sharif Shamba iliyopo manispaa ya Ilala ambapo ITV
imefika katika eneo hilo na kukuta kituo kikiwa kimefungwa huku kukiwa
na tangazo kubwa Linalosema uchaguzi wa mwenyekiti wa serikali ya mtaa
utafanyika tarehe 21 mwezi huu, ambapo baadhi ya wakazi wa maeneo hayo
wakiwemo wagombea wamelalamikia kupotezewa muda baada kutokana na kufika
mapema kutuoni
Hapo.
Aidha kufuatia vurugu zilizojitokeza katika kituo cha Kinondoni
mjini na baadhi ya watu watatu wamekutwa na masanduku manne ya kupigia
kura na kufanya uchaguzi kua, kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa
Kinondoni kamilius wambura amesema jeshi la Polisi linawashikilia watu
watatu kwa mahoajiano zaidi kutokana na kukutwa na karatasi hizo.
Aidha katika kituo cha Mivumoni kata ya wazo Tegeta, kituo cha
Mikocheni na kituo cha mtaa wa Bwawani Mwanamyamala idadi kubwa ya
wananchi wamejitokeza kupiga kura bila ya kuwepo kwa tatizo lolote la
vifaa huku ulinzi ukioekana Kuimarishwa katika maeneo yote ambapo baadhi
ya wananchi wamewataka wagombea kukubaliana na matokeo kutokana na
uchaguzi huo kufanyika kidemokrasia na kufuata kanuni.
- Itv
Post a Comment