![](http://www.itv.co.tz/media/image/MAJAMBAZI14.jpg)
Jeshi
la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwauwa majambazi sita waliokuwa
wanapanga kuteka mabasi katika eneo la ngazi saba wilayani Biharamulo.
Akizungumza mkoani Kagera kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Henri
Mwaibambe amesema jeshi la Polisi lilipata taarifa ya kwamba kunakundi
la majambazi linafanya mpango wa kuteka magari na kufanya uporaji katika
eneo la ngazi saba wilayani Biharamulo ambapo jeshi hilo lilifanya
doria na kufanikiwa kuwauwa majambaizi sita.
Kamanda Mwaibambe ameongeza kuwa kati ya majambazi hao sita ni
mmoja tu aliyetambulika kwa jina Gahungu Gerad raia wa Burundi na
wengine watano bado hawajafahamika.
Hata hivyo kamanda Mwaibambe ametoa onyo kwa wahalifu mbalimbali
kwa kuwataka waache kabisa kufanya vitendo vya uhalifu kwani serikali
inamkono mrefu wakiutawala na kwamba jeshi la Polisi sasa limeimarisha
ulinzi katika mapori ya Kasindaga na Biharamulo kwa lengo la kudhibiti
majambazi wanao ingia kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi na Uganda.
- ITV
إرسال تعليق