Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
--
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzialeo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba
kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow
hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Weremakwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu
na uadilifu.
إرسال تعليق