KASULU WAAHIRISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI ya wilaya ya Kasulu imeahirisha zoezi la upigaji kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa kufuatia kuwepo kwa dosari kubwa kwenye karatasi za kupigia kura ambazo zisingeweza kutoa ushindi wa haki kwa wagombea.
kuahirishwa kwa kikao hicho kunafuatia kikao cha pamoja baina ya wasimamizi wa uchaguzi wilayani humo,viongozi wa vyama na wagombea ambao wamekubaliana kwa kauli moja kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu,Masalu Mayaya ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi katika wilaya hiyo amethibitisha kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana na dosari zilizojitokeza.
Mayaya alizitaja kasoro zilizojitokeza kuwa ni pamoja na kuchanganyika kwa majina ya wagombea na nembo za vyama vyao ambapo majina ya mgombea mmoja yameenda kwenye nembo ya chama kisicho chake.
Sambamba na hilo Mkurugenzi huyo alisema kuwa pia kumekuwa na upungufu wa karatasi za kupigia kura katika baadhi ya vituo na hivyo kusababisha watu wengi kutopiga kura.

Post a Comment

Previous Post Next Post