HALMASHAURI ya wilaya
ya Kasulu imeahirisha zoezi la upigaji kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wa
serikali za mitaa kufuatia kuwepo kwa dosari kubwa kwenye karatasi za kupigia
kura ambazo zisingeweza kutoa ushindi wa haki kwa wagombea.
kuahirishwa kwa kikao
hicho kunafuatia kikao cha pamoja baina ya wasimamizi wa uchaguzi wilayani
humo,viongozi wa vyama na wagombea ambao wamekubaliana kwa kauli moja
kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu,Masalu Mayaya ambaye ndiye msimamizi wa
uchaguzi katika wilaya hiyo amethibitisha kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana
na dosari zilizojitokeza.
Mayaya alizitaja
kasoro zilizojitokeza kuwa ni pamoja na kuchanganyika kwa majina ya wagombea na
nembo za vyama vyao ambapo majina ya mgombea mmoja yameenda kwenye nembo ya
chama kisicho chake.
Sambamba na hilo Mkurugenzi huyo alisema kuwa pia kumekuwa
na upungufu wa karatasi za kupigia kura katika baadhi ya vituo na hivyo
kusababisha watu wengi kutopiga kura.
إرسال تعليق