Baba Askofu Methodius Kilaini akitoa huduma kanisani.
UKIHOJI dhambi za viongozi wa dini harakaharaka
utaambiwa fuata mafundisho yao usifuate matendo. Hili ni kinyume na
Mtume Paul aliyefundisha waumini wake kuwa wamfuate yeye kama
alivyomfuata Yesu.
Kwa kuwa dini ni muhimu kwenye kaya yangu sibishi sana katika hilo,
lakini kuhusishwa kwenye fedha chafu kwa viongozi wa dini Askofu
Methodius Kilaini, Euesebius Nzigirwa na Alphonce Twimannye
kumenibadilisha mtazamo.
Sikuwahi kuuliza utakatifu wa viongozi hao wa dini kwa sababu za
kutofuata matendo yao; lakini sakata la ufisadi wa Escrow wa zaidi ya
shilingi bilioni 300 limenifanya nijiulize kimoyomoyo watawa hawa
walipewa fedha hizo kwa ajili ya kazi gani?
Swali hili lipo na litaendelea kuwepo kwa sababu Mkuu wa Kaya sijapata majibu ya msingi. Kwa hali hiyo, hata nitakapokwenda kuungama dhambi zangu mbele ya watumishi hao wa Mungu nitakuwa nawatazama usoni.

Ukweli ni huo; nitakuwa natubu dhambi
zangu lakini wakati huohuo nayauliza mapaji ya uso ya viongozi hao
kulikoni wakajichotea mamilioni ya fedha ambazo hazina utakaso?
Nitafanya hivyo kwa sababu utetezi unaoenezwa juu ya watawa hao kuhusu
kupewa fedha za Escrow haujanikata kiu. Nafikiri siyo mimi tu, ni pamoja
na wanazengo wenzangu katika kaya hii.
Askofu Euesebius Nzigirwa(wa pili kulia) akiingia kanisani.
Askofu Euesebius Nzigirwa(wa pili kulia) akiingia kanisani.
Wapo wanaosema kuwa viongozi hao wa dini walipewa mamilioni hayo kama
sehemu ya sadaka. Swali langu; lini sadaka ya kanisa akapewa kasisi na
siyo kuwekwa kwenye kapu la makusanyo kanisani?
Nasisitiza; nitaungama nawatazama usoni. Nitafanya hivyo kwa sababu hata kama wao ni sehemu ya kanisa na kwamba inawezekana walitumwa kidini kupokea fedha hizo, vipi kanisa husika halijatoa kauli ya kutambua sadaka hiyo mpaka leo?

Hahaha...inachekesha kiasi pale wengine wanapoibuka na utetezi kuwa,
watumishi hao wa Mungu walipewa fedha hizo kama msaada wa kiutu. Swali;
msaada kwa ajili ya dhiki gani wanazokabiliana nazo watawa hao waliopewa
kibali na maandiko kuwa wale kupitia huduma zao.
Kama nilivyosema; sitaacha kutubu kwao kwa sababu ya umuhimu wa ibada
lakini suala la kuwatazama usoni sitaliacha mpaka nitakapopewa mantiki
ya kutofanya hivyo. Nafikiri hata mjukuu wangu mkubwa kaniambia
anasubiri jibu.
Hata kama sikusoma sana mambo ya dini lakini najua kuwa huduma za
kiroho hutolewa bure, hivyo kuifanya sababu ya kuwepo kwa malipo ya
kiroho kukosa mashiko. Na isitoshe maandiko yanaonya kuwa huwezi
kutumikia mabwana wawili kwa maana ya Mungu na mali. Hii ina maana
kwamba, siyo sahihi pia kwa watawa kuwa ‘wachuuzi’ kwa kisingizio cha
kupata fedha za kusaidia waumini wao, kwa sababu kazi ya ulezi ni ya
kanisa kuu siyo padri wala askofu pekee.
Kwa hoja hizo msimamo wangu ni kuwa, nitakwenda kanisani, ila wakati
wa kuungama nitakuwa nawatazama usoni wanaoniungamisha madhambi yangu ya
ulevi, matusi, wivu na chuki.
Nitafanya hivyo huku najiuliza wanitoweje kibanzi kwenye jicho langu wakati wao wana boriti machoni? Mkuu wa Kaya nimeishiwa uvumilivu katika hili; wakitaka nifute msimamo wangu wajitakase na wao kwenye sakata la Escrow bhaanaaa!

Kama hilo halitoshi, kwa kuwa mimi ni Mkuu wa Kaya namuomba sana mkuu
wa kanisa atoe tamko kuhusu watumishi hawa wa Mungu ambao hawakutajwa
kwenye adhabu zilizopendekezwa na bunge, ambapo mimi nawasilisha
maazimio ya wananzengo wenzangu kuwa, viongozi hao wa dini wavuliwe
nyadhifa zao. NA HOJA HIYO IMEUNGWA MKONO!
إرسال تعليق