![news inscription in studio tv](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/12/online-news.jpg?resize=407%2C270)
Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu alisema kuwa ameamua
kuchukua uamuzi huo baada ya kwenda katika Kata ya Kinungu na kuambiwa
na wananchi kuwa mtendaji huyo ana zaidi ya miezi miwili hafiki katika
kituo chake cha kazi.
“Ndugu zangu wajumbe mliohudhuria kikao hiki naomba mniunge mkono kwa
maamuzi niliyochukua mimi nilikwenda Kata ya Kinungu kukagua ujenzi wa
maabara lakini cha ajabu nilikuta wananchi wakilalamika kuwa mtendaji
Mapalala hayuko kituoni kwake kwa zaidi ya miezi miwili,” alisema.
Aidha Kingu alidai kuwa haiwezekani mtumishi wa Serikali akapokea
mshahara wa bure pasipo kufanya kazi ya serikali na kushindwa kusikiliza
wananchi.
Alisema kinachoshangaza mtendaji huyo amekuwa akishinda mjini akila
bata na kuku pamoja na kunywa pombe huku Mkurugenzi na Ofisa Utumishi
wakimfumbia macho pasipokuchukua hatua yoyote dhidi yake.
Alisema kutokana na hali hiyo yeye kama Mkuu wa Wilaya ya Igunga
hayuko tayari kuwa na watumishi wazembe hivyo amemuagiza Mkurugenzi
kumchukulia hatua kali mtendaji huyo.
Sambamba na hayo, Mkuu huyo wa Wilaya ameliagiza Jeshi la Polisi
Igunga kumkamata mtendaji Mapalala na kumfungulia mashtaka ya kula
mshahara wa serikali pasipo kufanya kazi.
Post a Comment