Rais Barrack Obama wa marekani amefananishwa na tumbili wa msitu wa Tropiki
Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na matatizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita.
Tume
ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani
inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananishi rais wa
marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na
kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa ka filamu yenye utata
inayojulikana kama The Interview.
Filamu ya the interview ambayo rasi Obama alishinikizwa ionyeshwe
Filamu hiyo iliyotengenezwa na
kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa
korea kaskazini Kim Jong Un. Korea kaskazini imekana kuhusika
kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni
hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.(BBC)
Post a Comment