Lulu:- Kuwa Mama ni Heshima Sio Kuzeeka, Nipo Njiani

Mrembo na mwigizaji wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael “LULU” ameamua kufunguka na kusema mtazamo wake kuhusu swala la wasichana kuogopa/kukataa kuzaa kwakuofia kuwa watazeeka.
“Kwa akili Yangu ndogo... Nadhani kuwa Mzazi(Mama)ni heshima kubwa na Sio kuzeeka kama wasichana wengi wanavyofikiria....! Shout Out kwa Kila mwanamke aliyefanikisha kupata Heshima Hiyo...! Heshima kwa Mama wote Duniani ….Wengine Tuko njiani Inshallah” Lulu aliweka bandiko hilo mtandaoni  baada yakuweka picha ya msanii  wamziki wa marekani, Ciara akiwa na mtoto wake wakiwa wamevalia kofia za “Christmas”.
Watu wengi walimpongeza kwa bandiko hili na hizi ni 'comment' kutoka kwa  Aunt Ezekieli na Zamaradi Mtetema.
Aunt Ezekiel:  Toka nimekufahamu leo ndio umeongea point toto akee... Kina mama Oyeeeeeee
Zamaradi Mtetema: Hasara.. baba yule!!! Hahahahaha uko tayari kwa ule mwendo!??
Lulu: @zamaradimketema ntauvumilia tu bwahahahahah
Na wewe ongeza yako hapo chini

Post a Comment

Previous Post Next Post