Penniel Mwingilwa.
Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel
Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume
wa kuzaa naye.
Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa Siku ya (Alhamisi)
na gazeti la Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo
lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza nasi hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi
anapomuona mtoto anachanganyikiwa na
kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi.
kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi.
“Kiukweli sasa ndiyo ule wakati wa kuzaa, natamani sana mtoto lakini
sasa wa kuzaa naye yuko wapi? Hapo ndiyo tatizo maana siyo kuzaa na mtu
ili mradi mtoto awe na baba,” alisema Penny
Post a Comment