Luke Somers raia wa Marekani mwandishi wa habari anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda huko Yemen
Marekani
imeeleza kuwa ilijaribu kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke
Somers, anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda nchini Yemen.
Rais Barack Obama aliidhinisha kikosi cha kumwokoa Luke, mwezi uliopita.
"Kwa
masikito, Luke hakuwepo, japokuwa mateka kutoka mataifa mengine
walikuwepo na waliokolewa," Baraza la Usalama la Taifa, limesema.
Mtu
anayejitambulisha kama Luke Somers, ambaye alitekwa mwaka 2013,
ameonekana katika video, akisema maisha yake yako hatarini na anaomba
msaada.
Video hiyo pia inamwonyesha mfuasi wa al-Qaeda huko Yemen
akitishia kumuua Bwana Somers hadi madai yao ambayo hayajatajwa,
yatakapotimizwa.
Bwana Somers, mwenye umri wa miaka 33,
alifanyakazi kama mwandishi wa habari na mpiga picha wa mashirika ya
huko na kazi zake zikaonekana katika vyombo vya habari vya kimataifa,
ukiwemo mtandao wa BBC.
إرسال تعليق