MATUKIO KIGOMA:_Kaburi Lakutwa Limefukuliwa Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.

Kundi la watu wasio fahamika wamelifukua kaburi moja Wilayani Kibondo na kufanikiwa kufungua sanduku la Marehemu upande wa kichwani na kulitelekeza kaburini.
Akizungumza Katika tukio hilo Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Wilayani Kibondo Inspecto. Peter Makala amemtaja marehemu  kuwa ni Merania  Mankanga Kikoko anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 83 Makazi wa Kijiji cha Bitale.


Tukio hilo limetukia November 28 mwaka huu majira ya saa 11:00 asubuhi ambapo ndugu wa marehemu  walio chelewa zoezi la Mazishi walipokwenda kutembelea kaburi hilo katika eneo la Makaburi ya MaLagarasi ,kIsha Walikuta kaburi likiwa limefukuliwa.
Aidha Mwenyekiti wa Kitongoji cha MaLagarasi Bw. Daniel Mahanga amesema tukio hilo ni la kwanza kutokea katika eneo hilo na kusisitiza kuwa jeshi la polisi linatakiwa kufanya upelelezi wa kina ili kuweza kuwatia nguvuni waliohusika katika tukio hilo.

 CDT...kibondomotoblog

Post a Comment

أحدث أقدم