Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe, Lucas Mweri.
Hayo yalielezwa na Afisa ustawi wa jamii Wilaya ya Korogwe, Jerome Mbonde, wakati akiwahutubia wananchi kwenye maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini hapa.
Mbonde aliyemwakilisha mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Lucas Mweri, alisema wazazi hawana budi kujenga uvumilivu kwenye ndoa zao wakitambua kuwa watakaoathirika na kutengana kwao ni watoto.
Hata hivyo, alitaja viashiria mbalimbali vya ukatili wa kijinsia kuwa ni wivu kwa wanandoa, umasikini ikiwemo utumikishwaji kwa mtoto na mimba za utotoni na kuitaka jamii kuvunja ukimya na kuhakikisha kila mmoja anashiriki kkamilifu katika mapambano ya kupinga matendo hayo kwenye maeneo yao.
Kwa upande wa dawati linaloshughulikiwa ukatili wa kijinsia, Mbonde aliwashauri maofisa wa dawati hilo kupanua wigo na kufungua ofisi za kutoa huduma kwa wahanga kila maeneo ili wananchi waweze kunufaika na mpango huo unaoendeshwa chini ya jeshi la polisi.
Awali akisoma risala ya dawati hilo kwa mgeni rasmi, Mariam Shaban alisema kuwa lilianzishwa wilayani humo mwaka 2011 na jumla ya makosa 200 yaliyohusu ukatili na unyanyasaji wa kijinsia yaliripotiwa.
Alisema kesi 170 zilifikishwa mahakamani ambapo 10 kati ya hizo zilishinda na 20 zipo chini ya upelelezi wa dawati ambapo kwa mwaka 2014 zimeripotiwa kesi za aina hiyo 99.
Alisema kati ya hizo 89 zimepelekwa mahakamani, 50 zimeshinda.
Aidha alitaja changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao kuwa ni pamoja na kukosa usafiri, fedha, ufinyu wa ofisi, thamani za ndani na tatizo la wananchi kutoa ushirikiano mdogo katika ushahidi mahakamani kwa lengo la kuwalinda wahalifu.
Mratibu wa dawati la polisi Wilaya ya Korogwe, Aneth Malekela, alieleza kuwa katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa Wilaya ya Korogwe, dawati linashirikiana na Idara ya Ustawi wa Jamii, mashirika, mahakama, idara ya afya na taasisi zisizo za kiserikali.
Malekela alisema kutokana na changamoto hizo dawati limeshindwa kujitanua kwani limefungua ofisi katika vituo vya polisi vitatu kati ya tisa vilivyomo wilayani humo na ambapo kunahitajika msukumo mkubwa ili kuliwezesha kufika kwenye vituo vyote.
CHANZO:
NIPASHE

إرسال تعليق