Stori: Imelda Mtema KWELI
kifo hakina huruma jamani! Mshiriki wa Miss Tanzania 2013 akitokea Miss
Ilala, Martha Gewe, mkazi wa Tabata Segerea, Dar amefariki dunia baada
ya kuugua ghafla, Ijumaa Wikienda linakupa zaidi.
![](http://api.ning.com:80/files/Ktsylelmf0mneSNCWwk5WOEPgFDf1LQIU4sMKBB6VN0nYpFUM*KSL3UY6MGcpw83z3aRHk2YzrARXHD*hoSbNWJzdUIcPxg9/IMG20141213WA00071.jpg)
AFYA YAKE SIKU ZA NYUMA
Habari zaidi zinasema kuwa mrembo huyo hakuwa akisumbuliwa na ugonjwa wowote huko nyuma na alionekana mwenye afya njema huku mipango yake ikiwa imelenga jinsi atakavyoisherehekea Sikukuu ya Krismasi.
“Lakini Jumatano iliyopita alianza kuumwa, alisema anahisi homa ambayo baadaye ikabainika ni malaria.
![](http://api.ning.com:80/files/Ktsylelmf0kBTUPa*8wmETvdHiLVw8ACQhcSRd6biSdQ03yX3yCklig1y4kGqgsXPso04qWlhdVLw9qjoOjmS17xl71BNtEr/IMG20141213WA00041.jpg?width=650)
WALICHOSEMA MADAKTARI
Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kuzungumza na madaktari wawili wa Hospitali ya Amana jijini Dar kuhusu ugonjwa wa malaria kupanda kichwani.
Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kuzungumza na madaktari wawili wa Hospitali ya Amana jijini Dar kuhusu ugonjwa wa malaria kupanda kichwani.
![](http://api.ning.com:80/files/Ktsylelmf0lfKcf3olMKuOYMF6j6cXOWgJsnvyuzJrH7nJtlb2tsDQYc9qhZifWXgPVzoxrPEhRPRhAn5am3tqOObe98VVJ5/IMG20141213WA00101.jpg?width=650)
“Kikubwa watu wazingatie kuwa mbali na mazingira hatarishi kwa ugonjwa huo na wajichunge kuumwa na mbu ambao ndiyo wana-oeneza ugonjwa huo,” alisema daktari mmoja.
MAMISI WENZAKE NI MACHOZI
Kufuatia taarifa za kifo hicho, mamisi wenzake walipigwa na mshangao, wengine wakiuliza nini kilimpata mwenzao huyo!
Kufuatia taarifa za kifo hicho, mamisi wenzake walipigwa na mshangao, wengine wakiuliza nini kilimpata mwenzao huyo!
![](http://api.ning.com:80/files/Ktsylelmf0mOyxqOuACKY9pmYGAzOLAnFMNKoPRuGyl3hGpN0vy4j1xPU9y7znqpYO-493uOnCFqNjq4Cw5FK11oIM*rKdeE/watimanywa.jpg?width=650)
“Kifo chake kimeniumiza sana, sijui hata nisemeje jamani, kweli kifo hakina huruma,” alisema Miss Ilala 2013, Dorice Mollel huku akilia.
Mrembo mmoja ambaye hakutaja jina lake alisikika akisema: “Yaani Happiness (Watimanywa) yuko Uingereza kusaka taji mwenzake anapoteza maisha ghafla hapa nyumbani Tanzania! Inauma sana kwa kweli.”
Warembo wengine walioshiriki msiba wa Martha nyumbani kwao, Tabata, Dar walishindwa kujizuia na kujikuta wakibubujikwa machozi muda wote kiasi cha kushindwa kuongea na mwandishi wa gazeti hili.
![](http://api.ning.com:80/files/Ktsylelmf0n6Zjs-vhGCZwi147O*AKyJHgOpbesjkZdBEUkKCVOUNBvyHWLzfxiR-*1w1jhRs5ASaEgcs2MhHvv5oFbaTJbh/HashimLundenga.jpg?width=650)
Mwaka jana, Martha alishiriki shindano la kumsaka Redd’s Miss Ukonga lililofanyika katika Ukumbi wa Wenge Garden, Ukonga Mombasa jijini Dar.
Katika kinyang’anyiro hicho, Martha
aliibuka kidedea kwa kuvalishwa taji hivyo kupata tiketi ya kwenda
kushiriki Miss Ilala 2013 kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar
ambapo mshindi alikuwa Dorice.
Marehemu alipata nafasi ya kuvuka Miss Ilala na kushiriki Redd’s Miss Tanzania 2013 chini ya Hashim Lundenga ‘Anko’ na kufanikiwa kuwa miongoni mwa Kumi Bora huku Happiness Watimanywa akiibuka mshindi.
Marehemu alipata nafasi ya kuvuka Miss Ilala na kushiriki Redd’s Miss Tanzania 2013 chini ya Hashim Lundenga ‘Anko’ na kufanikiwa kuwa miongoni mwa Kumi Bora huku Happiness Watimanywa akiibuka mshindi.
![](http://api.ning.com:80/files/Ktsylelmf0lRcGbbjK2-ikbKEKHgbpLgZzrnWjUqmbtHfWnHzmWcAq3GoY1Pw904aNITH-QBnwBhK5H*1ltMEB2sJjPjjC3s/MISSTZ1.jpg?width=650)
MAZISHI YA MARTHA
Marehemu Martha alizikwa Jumamosi iliyopita kwenye makaburi ya nyumbani kwao, Tabata Segerea jijini Dar es Salaam huku msiba huo ukihudhuriwa pia na warembo mbalimbali ambao wamewahi kuvaa mataji nchini.
Post a Comment