MSIMU WA SIKUKUU LE MBEBIZ IMEKULA KIPANDE YAKE

Oya masela inakuwa nini kwa kitaa hiyo? Ni mzuka? Kipande hii ni mpango mzima. Mambo vipi hapo kwa wanangu Wanyalu kwa fasi ya Iringa? Basi barida machalii wangu!
Hivi washkaji yale mangawira ya eskro ndo imetoka au? Maana naona mafisadi waliotuhumiwa wanadunda tu kitaa wakati maraia wanasafa kinoma. Ni mwendo wa kuungaunga wakati wao wanapeta mwanzo mwisho.
Kama vipi tukomae hadi kieleweke! Wasiporudisha hakyanani neksti uchaguzi ndo tuwahukumu.
 Kama hawajasunuka wee wasubiri! Siyo faa. Si ni neksti yia tu? Hakuna kumpa ulaji fisadi hata kama watatupigia magoti.
Wakuu kitu cha mwaka ndo kinayoyoma, tupo kwenye dakika za lala salama. Hapa mshiko umekata na homu sijarekebisha chochote. Oya wanangu huko kwenu vipi? Punguzeni stresi, ongezeni spidi ya kuzimeki dheni kama ipo ipo tu!
Turudi kwa fasi ya jamvini kwetu hapa tuendelee kusebenza na mastori moo ya tauni. Ebana G ni mtoto mkare kinoma ambaye tumekuwa naye kitambo kwenye kusaka bingo. Anajua kutafuta siyo wale wa kubweteka tauni na kutegemea kuwapiga mameni. Siku hizi wanyama wao nao wamesanuka, wamekuwa bahili hatare!
Ni mwaka wa bee sasa G amekuwa na msela ambaye eviri mwaka anampromisi kwamba atamuoa bati deizi zinakwenda resi kinoma na wala jamaa hana mpango wa kurekebisha ishu hiyo. Anakula na kuinjoi tu wepesi na mambo f’lani kutoka kwa shori.
Mtoto mzuri anakatiza huku na huku ufukweni lasti wikiendi, akakutana na mtu mzima Mpeke akila bata za kiutu uzima. Si unajua zile za kudiliti mafaili baada ya kupiga kizigo mwaka mzima? Wazazi bata wapi?
Mbona hatukaribishani msimu wa holidei? Ngoja mimi niwakaribishe kwenye msimu wa sikukuu! Karibuni kama jasho la mtu laliwa.
Basi mtoto mzuri anakuteli kuwa jamaa yake amekuwa mtu wa kumpiga kalenda nini na nini.
Saundi kibwena arifu. Wakati mwaka huu unaanza msela wangu alimwambia G kwamba piga ua masti Desemba hii ampige na kitu cha mereji. Unajua shori masti umchiti ndo kieleweke.
Walahi usipomdanganya shori humpati daadeki utasaga soli sana.
Nawu mazee Desemba ndo hii na jamaa hana dalili za kumuoa mbebiz mkare zaidi ya kumpumbaza na bata ndefu. Yaani kila wikiendi masti wakajiachie kwa ufukweni au swimming puuli ilimradi tu wainjoi hili laifu fupi bila kuwaza fyucha chaliiangu. Huo si umbulula jamani?
G anakwambia yupo kwenye krosi rodi kinoma kozi taimu inamuvu fasta na eji nayo inakwenda. Sasa anakaribia kugonga kitu cha thelathini na mzazi jembe hana taimu ndo kwanza anaruka na mambo ya ujanki. Basi ukiona hivyo ujue mbebiz mkare imekula kipande yake.
So ndo kama hivyo mtoto mzuri ameona kama jamaa ni longolongo beta akampiga dauni dheni afaindi laifu lingine. Si umbo na sura bati mtoto ana mtaji mkubwa wa tabia na kichwani zipo za kutosha.
Ameenda kidato, shule imeseto kichwani. Ukiwa na shori kama huyo mazee laifu linataka nini tena? Naona msela haelewi kwamba mashori wa sampo hizo nawu deizi ni wa kumulika na tochi.
Kama vipi jamaa hakusomi so mpige dauni akija kushtuka wewe upo faa kinoma arifu. Hiyo ndo advaisi yangu kwake dheni ataamua yeye kama asuke au anyoe kiduku!Mmenisoma wanangu? Maduu wa tauni poleni. Sanukeni inakula kwenu! Kama vipi sii yuu neksti wiki! Nduki! 

Post a Comment

أحدث أقدم