Na Woinde shizza,Arusha
Hakimu
David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya maji ya chai ameahirisha hadi
december 24, shauri la kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arumeru
mashariki Joshua Nassari (CHADEMA), kwa tuhuma za kuharibu mali ya uma
kwa kuichoma yenye dhamani ya shilingi laki mbili (bendera ya
CCM),pamoja na kumteka mtu na kumtishia kwa bunduki tukio ambalo
anatuhumiwa kufanya december 15 mwaka huu
mahakama
hiyo imemuachia mbunge huyo mara baada ya kutimiza mashariti ya dhamana,
ambapo shariti la kwanza ni kuwa na wadhamini wa tatu ambao wanamali
zisizo hamishika zenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu kila
mmoja.
Katika
kesi hiyo inayomkabili mbunge huyo ambayo mlalamikaji wa kesi hiyo akiwa
ni mtu binafsi hakimu wa kesi hiyo mara baada ya kusikiliza mashitaka
hayo alichukuwa nafasi ya kuhairisha kesi hiyo adi december 24 ambapo
kesi hiyo itatajwa tena kwa mara nyingine.
Akiongea
mara baada ya kuairisha kesi hiyo wakili wa mbunge huyo wa Arumeru
mashariki James Ole milya alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio la
mahakama hiyo kumpa mashariti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa
haitaji mashariti makubwa hivyo .
Aidha
alisema kuwa mbali na kupewa mashariti hayo angependa kesi hiyo ipelekwe
katika mahakama ya wilaya ili yeye kama wakili wa mbunge huyo aweze
kumtetea kwani katika mahakama ya mwanzo hairuhuu kuweka wakili.
“unajua
kwakweli mbali na hivyo pamoja kuwa sio jamuhuri imemshitaki mh Nasari
bali ni mtu binafsi lakini nasikitika sana kwa mashariti ambayo wameweka
,kwani ata bila ao wathamini watatu wakiwa na kitu kisichoamishikika
chenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu,huyu ni mbunge ambapo
angeweza kujidhamini ata yeye mwenyewe kwani mtu huyu ni kioo cha jamii
na awezi kukimbia sehemu yoyote kwanini wasinge mpa mdhamana mapema
mpaka apate wadhamini hawa na mashariti haya”alisema Milya
Aidha
alisema kuwa anashangazwa sana na maamuzi haya kwani kuna mtu ambaye
amemzalilisha mwanamke ambaye alikuwepo mahakamani hapo na akamvua
mwanamke huyo nguo lakini yeye alishangazwa sana kwa mtuhumiwa wa kosa
ilo la uzalilishaji yeye kupewa mashariti mapesi ya kuwa na mdhamini
mmoja na kutoa laki tano laikini mbunge yeye amepewa mashariti ya kuwa
na wadhamini watatu ambao wanamalizi zenye dhamani ya shilingi milioni
moja na nusu uku akitilia shaka kuwa katika kesi hii wanahisi kuna chama
cha siasa kinachangia kuongeza nguvu.
Post a Comment