Mwenyekiti wa Nec, Jaji mstaafu Damian Lubuva.
Zoezi hilo litakuwa ni la kujiandikisha, kuweka alama za vidole, picha na kisha kutolewa vitambulisho litafanyika maeneo ya Bunju A na Mbweni, mkoani Dar es Salaam na Kilombero, mkoani Morogoro pamoja na Mlele katika mkoa wa Katavi.
Mmoja wa maofisa wa NEC aliliambia NIPASHE jijini Dar es Salaam kuwa zoezi hilo ni la majaribio ambalo litadumu kwa siku saba na zoezi rasmi litaanza Januari mwakani.
Alisema majimbo yaliyopangwa kufanyiwa zoezi hilo, litawasaidia wananchi kupata kitambulisho kitakachotumika kwenye uchaguzi mkuu.
“Zoezi hili la majaribio lilitakiwa lianze juzi, ila kutokana na muingiliano wa uchaguzi wa serikali za mitaa limechelewa na kuanza jana na litadumu kwa muda wa siku saba,” alisema.
Naye karani wa kuandikisha majina kituo cha Bunju A, Hawa Mpore, alisema zoezi hilo halikuwa na changamoto kwa siku ya kwanza kwani muitikio wa wananchi ni mzuri.
Naye Sunguru Chriss, mkazi wa eneo hilo, alisema zoezi hilo la uandikishwaji wa majina na upigaji picha ni zuri, ila wanaomba Mamlaka ya Vitambuliso vya Taifa (NIDA), ingetumia mfumo huo ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment