OYA MASELA KILEJI MOJA HIYO!


Inakuwaje wakali wangu wa nguvu? Masela barida? Basi kipande hii haina kwikwi chaliiangu. Ebana maandalizi ya kitu cha mnuso wa Eksimasi yakoje? Maana kama sielewielewi hivi. Naona pipo wapo bize kinoma hata hatupeani michongo kama ishu itakuwaje wazazi?
Tangu tulipomingo lasti wiki kumekrosi mambo kibwena hadi tudei tunamiti hapa jamvini. Kwanza kulikuwa na mchongo wa Mtani Jembe dheni zikaibuka ishu za mauchaguzi za serikali za kitaa. Ebana michongo yote bee imeacha makovu kwa baadhi ya wana. Tuweiti marizalti kamili ya haya mauchaguzi maana ni nouma aisee arifu. Ngoja nipige kimya nisije nikapigwa na kitu chenye ncha kali. Maana nawajua hawachelewi kunizimisha arifu!
Kama vipi tukomae na yale mangawira ya maeskro yarudishwe kwanza, hayo mengine yatajiseti tu daadeki. Nayamaindi yale mawe vibaya wanangu. Ooohoo…msione kimya mkadhani tumefogeti.
Hasahau mtu hapa kama mkituzingua mjue washikaji wanahaso kinoma kitaa so mtiti utakuwa uchaguzi ujao. Daadeki! Nipo tayari kuwashika masikio masela dheni kinuke hadi kieleweke! Kama hamtaki makuu rudisheni mawe ya maraia wavuja jasho! Hivi wewe una akili gani eti mtu akupe majifti ya mabilioni…kivipi? Kwa taarifa yako hata prezidaa mwenyewe alishasema ‘ukila masti na wewe uliwe’.
Kama vipi piga chini ishu za kiloko tupige mastori moo ya kitu cha holidei. Ebana unajua kuna tofauti kubwa kati ya holidei za wenye mawe na makabwela. Wenye nazo huwa wanakwenda vekesheni kama kwenye vivutio vya utalii duniani na plesi nyingine kama hizo.Kwa makabwela vekesheni ni kileji moja hiyo kwa ajili ya kwenda kuwapa hai maparenti, ndugu, jamaa na mafrendis.
Huko ndo kwetu. Kuna bonge la nukuu kuwa ‘msahau kwao ni mtumwa’. Unajua majanki wengi nawu deizi wakishatimba tauni na mambo yakinyooka kiduchu tu husahau walikotoka hasa kileji bati huo ni umbulula.
Hii ndo sizoni ya holidei. Ndo taimu pekee ya kwenda kwa kileji. Oya washikaji mi nipo rodini naelekea kwa fasi ya kileji moko hiyo.
Mazee laifu mdogomdogo na namshukuru Saa Godi kozi siku hizi Mpeke naye anakula kitu cha pipa kwenda kileji. Respekti iende kwa Team Mpeke. Jamaa wana lavu ya ajabu kwa jembe lao so wameona akienda kuwasabahi maparenti dheni akamate kitu cha pipa. Ni stepu kubwa kwenye hili laifu tafu.
Basi bana kwenye fasi ya eapoti tayari taimu ya kufunga belti imetimba. Kucheki pembeni ebana kuna bonge la mtoto mkare hatare. Duh! Nimeamini Bongo tambarare kuna makiksi wakali kinoma aisee.
Wewe tu na kawaleti kako. Kama kametuna ni mpango mzima kozi unabadilisha hadi neimu unaitwa Pedeshee Kifaranga Mutoto ya Kuku au Pedeshee Maprosoo. Chezea mawe wewe? Kama kamekondeana dheni mashori wote tauni utakuwa unawaita mashemeji.
Sasa kwenye pipa ili kushea aidia inabidi mwanaume ufanye fasta maana siyo kama basi useme utakaa taimu ndefu…unashangaa tayari kitu kimetua. Hapo ndo unaanza kujilaumu…ningejua…ningejua kumbe umeleiti. Chemka mwanaume!
Basi kaka mkubwa nikatafunatafuna maneno na yai langu linalogongagonga bati mwisho wa dei nikafanikiwa kukamata bizinesi kadi. Angalau mdogomdogo tayari mawasiliano yameanza na mazingira siyo mabaya sana. Taimu yoyote naweza kukamata fursa dheni twenzetu.
Masela kuanzia nawu nitakuwa napatikana kwa machale kinoma maana vekesheni hakutaki mastresi. Ni mwendo wa kuskani mafolda kuondoa vairasi na kuweka mikakati au softiweya ya neksti yia.
Wanangu msimisi hapa jamvini neksti wiki kozi nitawapa mamichongo kibwena ya msimu wa holidei dheni nitatoa bigi apu kwa wana wote tuliokuwa tunachati hapa jamvini kwa mwaka mzima.Mmenisoma masela? Kama vipi nawawishi maandalizi barida ya eksimasi. Sii yuu mameni na maduu. Nduki!

Post a Comment

Previous Post Next Post