NJEMBA ACHEZEA MAKOFI YA BAUNSA

KAMA kawa, kama dawa! Mapaparazi wetu wanaotii amri ya bosi wao, Musa Mateja ‘Toz’, Shani Ramadhani na Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ walisambaa katika viunga tofauti vya starehe na kuwasiliana moja kwa moja na mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Saa 4:00
Mkuu akiwa katika kiti chake cha kunesanesa, anaangalia saa na kugundua ni muda muafaka wa kuanza kuwacheki mapaparazi, anaanza na Musa Mateja:

NJEMBA ACHEZEA MAKOFI YA BAUNSA
Makao Makuu: Mateja leo sijisikii vizuri kiafya hivyo sihitaji kabisa kusumbuana na nyinyi sijui uje hapa ofisini nikuachie majukumu ya kuzungumza na wenzako?
Mateja: Haaa... una nini bosi wangu au bado unaugulia kichapo cha bao 2 kutoka kwa Simba?
Makao Makuu: Mateja huko ni kukosa nidhamu sasa hayo mambo ya Simba na Yanga yanatokea wapi wakati mimi niko siriasi na ninakwambia naumwa?

Mateja: Basi ‘am’sori mai bosi’, nilitaka kujua tu!
Makao Makuu: Acha upuuzi wako wewe, hebu niambie fasta ulipo kwa sasa na unachokifanya.
Mateja: Hapa nipo Cheetoz Lounge au wengine wamezoea kupaita Miti Mirefu hapa Sayansi, Kijitonyama.

Makao Makuu: Kuna nini leo hapo maana siku hizi burudani za hapo zimekuwa hazieleweki kabisa.
Mateja: Leo kuna burudani kutoka kwa Akudo Impact.
Makao Makuu: Duuh, hivi bendi hiyo bado ipo tu kwenye anga za burudani maana mara ya mwisho kuona burudani yao ilikuwa ni Mango Garden na Christian Bella alikuwepo siku hiyo.

Mateja: Kweli jamaa kama walipotea kimuziki ila kwa sasa wamerejea na hapa hawajakosa hata siku moja na mambo yao naona kama yanaenda vizuri.
Makao Makuu: Niambie kipya kilichojiri hapo sasa?

Mateja: Wakati naingia hapa nimeshuhudia kijana mmoja akiwasili hapa na warembo wawili, ambao amekuja nao kwenye bodaboda amekaa staili maarufu kwa jina la mishikaki, baada ya kushuka akaja hadi getini wale warembo wakalipa kiingilio wakaingia yeye akawa hana fedha sasa akawa analazimisha kuingia huku akisema yeye ni msanii wa Bongo Fleva hivyo anapaswa kupita bure.
Makao Makuu: Eeh nini kikafuata baada ya kusema hivyo au wamemruhusu kuingia?

Mateja: Mmh... hakuna aliyemtambua pamoja na mbwembwe zake zote amejikuta akichezea kibao kutoka kwa baunsa mmoja ambaye alitoka ndani na kukuta kijana huyo akimsaundisha mtu wa getini, yaani katoka nduki baada ya kulamba vibao vyake viwili sijui hata kituo chake cha kwanza kama kimekuwa karibu basi itakuwa Mwenge au Tegeta.
Makao Makuu: Hahahaaa... kweli kwa vibao vya baunsa lazima atakuwa kasimamia stendi ya Mwenge.
Mateja: Umeona eeh, ila pamoja na hilo kala hasara ya kuwapoteza warembo wake aliokuja nao maana wakati yanamkuta haya yote wao walikuwa tayari ndani na hapa nawaona wanaserebuka bila hata habari.

Makao Makuu: Chezea warembo wa mjini wewe, huyo itakuwa imekula kwake ki mtindo huo na ukiwafuatilia hadi mwisho si ajabu ukaona wanatoka na Wakongo wa Akudo baada ya burudani kumalizika.
Mateja: Yawezekana ikawa hivyo kweli bosi kama vipi ngoja na mimi niwaangalie hadi mwisho nione mwisho wa siku watafanyaje.
Makao Makuu: Basi sawa kijana wangu.
Mateja: Haina noma bosi wangu.

Saa 5:48 usiku.
AKABIDHIWA MAJI NA DEKIO BAADA YA KUTAPIKA
Makao Makuu:  Habari ya muda huu Shani, leo kiwanja wapi?
Shani: Salama Mkuu nipo maeneo ya Kigamboni kwenye Baa ya Blue Fish.
Makao Makuu: Hee! Umeenda kula samaki huko, lakini kumbuka kazi ni muhimu kijana. Haya nipe ripoti.
Shani: Hapana Mkuu maeneo haya yana vituko sana hapa kuna mteja amelewa anatapikia watu hovyo.
Makao Makuu:  Mh...au ni mgonjwa?   

Shani: Siyo mgonjwa, ila anasema ndiyo anaianza sikukuu sasa anashangaa kuona mambo yanakuwa mabaya mapema. Sasa mhudumu naye kamjia juu amemkabidhi maji na dekio asafishe huku amesimamiwa.
Makao Makuu: Hiyo sasa ni funga mwaka kipindi kama hiki wengi sasa watahamia baa kabisa. Sasa ngoja niongee na Mkude Simba hapa naona ananipigia.
Saa 7:00 usiku
WASUTANA UKUMBINI
Makao Makuu: Shekidele  funguka fasta habari za Morogoro lakini?
Shekidele: Duuh! Mkuu hiyo kali, hata salamu?
Makao Makuu: Acha mbwembwe, haya niambie mzima? Leta maneno.
Shekidele: Mkuu nilikuwa katika oparesheni maalum ya kusafisha machangu kwa kushirikiana na jeshi la polisi na sasa nimeshamalizana nao nipo katika Ukumbi wa King Tom Pub, Bendi ya Maisha Mapya inakamua vilivyo.

Makao Makuu: Safi picha nazitaka hizo za machangu, enhe hapo kuna tukio gani umelinasa?
Shekidele: Hapa kuna wadada nimewakuta wanasutana ukumbini karibu kabisa na spika, ngoja niwasogelee nikujuze moja kwa moja.

Makao Makuu: Fasta wewe mimi leo siko poa.
Shekidele: Tayari nishawakaribia Mkuu, ishu ni kwamba kuna dada mmoja alikuwa anadaiwa fedha za marejesho ya mkopo sasa aliwatesa wenzake kwa kuingia mitini ndo mmoja wa wenzake akamkuta humu ukumbini na kuanza kumsuta.

Makao Makuu: Mkuu hapa ni balaa na kilichompa zaidi hasira ni baada ya mwanamke huyu kukutwa anakunywa bia wakati wenzake wamezichanga hadi kumlipia deni lake.
Makao Makuu: Hahaha poa wafuatilie kwa makini kama wakikunjana tupate picha, halafu ukimaliza waambie wenzako mkalale.

Post a Comment

Previous Post Next Post