Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipangoimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango ikiendelea na kazi ya ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Ujenzi unaendelea! Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo
la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kagera.
Pichani ni muonekano mpya wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kagera
kujionea maendeleo ya Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja hicho. Waliotangulia mbele ni
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja
cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Katikati) na Meneja wa kiwanja
hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia).
Wahandisi Pius Gobolo (kushoto), (Mhandisi Mshauri
wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba) na Suleiman Athuman (watatu kulia), Meneja
Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba wakitoa maelezo mara
walipoingia kwenye sehemu ya abiria ya jengo jipya la kiwanja hicho.
Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana
(Kulia) akifafanua jambo kwa Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wanaoshuhudia
ni Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman
Athuman (Wapili kushoto) na Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi
Pius Gobolo (Kushoto).
Hadi kuleeee.. Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius
Mulungwana (Mbele) akimuonesha Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia)
sehemu inayopendekezwa kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba. Picha na Saidi Mkabakuli-Ofisi ya Rais,Tume ya Mipango
---
Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani wataanza
kujivunia uwanja wa ndege wa kisasa kufuatia kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege
cha Bukoba.
Post a Comment