Vurugu ya aina yake imetokea kwenye ofisi
za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini baada ya Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo Chadema kushinda kwa kishindo katika kata ya Ngokolo hali
iliyosababisha viongozi wa ngazi za juu wa w CCM kuanza kushikana uchawi kwamba
nani kasababisha anguko hilo.
Malunde1 blog inaambiwa kuwa jana katibu
wa siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Charles Shigino almanusura
watwangane makonde na kuishia kutukanana matusi ya nguoni na katibu wa umoja wa
Vijana wilaya ya Shinyanga Mjini (UVCCM), Zawadi Hussein.
Varangati hilo lilitokea wakati Shigino
akiingia katika ofisi za chama hicho ambapo ghafla alitokea katibu wa umoja wa
vijana (UVCCM Hussein na kumzuia kuingia katika ofisi hizo na kuanza kumrushia
maneno machafu akimtuhumu kuchangia kufanya vibaya kata ya Ngokolo ambapo Chadema
wamepata ushindi katika mitaa 6 na CCM mtaa mmoja tu.
“Wakati
naendelea kujitetea, aliendelea kuporomoshea matusi mfululizo ,ndipo
uzalendo ukanishinda na mimi nikaanza kujihami na kusababisha
ugomvi mkubwa nje ya ofisi ya chama, na kujaza umati wa watu
wakishuhudia
ugomvi huu, ambao hauna maana zaidi ya kukiaibisha chama”,Shigino
aliiambia
Malunde1 blog.
Katibu wa umoja wa Vijana wilaya ya
Shinyanga Mjini Zawadi Hussein amesema alimzuia Shigino kuingia katika ofisi za
chama hicho kwa madai kuwa yeye ni msaliti wa chama na amekuwa akitoa siri na
kuzipeleka kwa wapinzani.
Katika uchaguzi huo wilaya ya Shinyanga Mjini kati ya mitaa 55 CCM, wamepata mitaa 26, CHADEMA mitaa 29.
Post a Comment