JOTO LA USHINDI WA CHADEMA VIONGOZI WA CCM SHINYANGA WATUKANANA NA KUTAKA KUPIGANA.


Vurugu ya aina yake imetokea kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kushinda kwa kishindo katika kata ya Ngokolo hali iliyosababisha viongozi wa ngazi za juu wa w CCM kuanza kushikana uchawi kwamba nani kasababisha anguko hilo.
Malunde1 blog inaambiwa kuwa jana katibu wa siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Charles Shigino almanusura watwangane makonde na kuishia kutukanana matusi ya nguoni na katibu wa umoja wa Vijana wilaya ya Shinyanga Mjini (UVCCM), Zawadi Hussein.
Varangati hilo lilitokea wakati Shigino akiingia katika ofisi za chama hicho ambapo ghafla alitokea katibu wa umoja wa vijana (UVCCM Hussein na kumzuia kuingia katika ofisi hizo na kuanza kumrushia maneno machafu akimtuhumu kuchangia kufanya vibaya kata ya Ngokolo ambapo Chadema wamepata ushindi katika  mitaa 6 na CCM mtaa mmoja tu.
“Wakati  naendelea kujitetea, aliendelea kuporomoshea matusi mfululizo ,ndipo uzalendo ukanishinda na mimi nikaanza kujihami na kusababisha ugomvi mkubwa nje ya ofisi ya chama, na kujaza umati wa watu wakishuhudia ugomvi huu, ambao hauna maana zaidi ya kukiaibisha chama”,Shigino aliiambia Malunde1 blog. 
Katibu wa umoja wa Vijana wilaya ya Shinyanga Mjini Zawadi Hussein amesema alimzuia Shigino kuingia katika ofisi za chama hicho kwa madai kuwa yeye ni msaliti wa chama na amekuwa akitoa siri na kuzipeleka kwa wapinzani.

Katika uchaguzi huo wilaya ya Shinyanga Mjini kati ya mitaa 55 CCM, wamepata mitaa 26, CHADEMA mitaa 29.

Post a Comment

أحدث أقدم