Baadhi ya askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
waliokosa ajira, wakimsikiliza ofisa wa polisi aliyewataka waondoke
eneo la Ocean Road jijini Dar es Salaam baada ya kufanya maandamano ya
amani kutoka Jangwani kuelekea Ikulu kwa lengo la kuiomba serikali
iwapatie ajira ya kudumu.
Vijana haa ni waliopitia operesheni Mkapa, Utandawazi, Jiajili, Miaka 40, Kasi mpya, Maisha bora, Uadilifu pamoja na Kilimo kwanza toka mwaka 2000 hadi 2014.
Vijana hao zaidi ya 300 walianza maandamano hayo saa mbili asubuhi kutoka Jangwani kuelekea Ikulu wakiwa wamebeba bendera zenye rangi nyekundu na vyeti walivyohitima mafunzo yao na walipofika eneo la Hospitali ya Ocean Road, polisi walizuia maandamano hayo na kuwataka kuchagua viongozi watakao wawakilisha.
Askari hao waliwataka wengine kuondoka eneo hilo na kutafuta eneo lenye usalama kwenda kuwasubiri viongozi wao watakapotoka Ikulu na kuwaletea majibu.
Mmoja wa kiongozi wa mafunzo, Magesa Maijo, alisema lengo la maandamano yao ni kupeleka kilio chao kwa Rais kutokana na kutopewa majibu sahihi kwa wizara husika.
CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق