Baadhi ya watu wenye ulemavu wanathibitisha kuwa ulemavu si kikwazo cha binadamu kutafuta haki ya msingi ya kupata elimu.
Tukiwathamini wenzetu wenye ulemavu na kuwajengea
mazingira rafiki ya kujiendeleza kielimu, wengi wanaweza kufika mbali
kielimu kama alivyo Profesa Edward Bagandanshwa wa Chuo Kikuu cha
Sebastian Kolowa (Sekomu), aliyeipata hadhi hiyo ya juu kitaaluma hivi
karibuni.
Profesa Bagandanshwa anathibitisha kuwa ulemavu si tiketi ya kukwepa elimu kama alivyohojiwa na mwandishi wetu.
Swali:Tueleze historia yako na namna ulivyopata ulemavu wa macho?
Jibu: Nilizaliwa mwaka 1959 katika kijiji cha Kaibanja Bukoba Vijijini, umbali wa kilomita 56 kufika Bukoba mjini. Ni mtoto wa pili katika familia ya Daudi Bagandanshwa na mkewe Apeneto Mbeoma. Nilipofikisha miezi sita baada ya kuzaliwa, nilikumbwa na maradhi ya surua na kwa kuwa wakati huo hakukuwa na chanjo, ikaharibu kabisa jicho langu la kushoto nikabaki na jicho moja la kulia.
Miaka saba baadaye wiki ambayo nilikuwa nimeandikishwa shule, nilikwenda kuchunga ng’ombe kama kawaida, ndipo mwenzangu aliporusha mshale na kunichoma jicho langu la kulia. Nilikimbizwa hospitali ya Ndolage na kufanyiwa operesheni kwa muda wa saa tano, lakini madaktari walisema nisingeweza kuona tena.

Swali: Ulipata ulemavu ukiwa tayari umeshaandikishwa shule, nini kilifuatia baada ya hapo?
Jibu: Ilipojulikana dhahiri
kwamba sitoona tena, kanisa likaamua kuchukua jukumu la kufanya jitihada
za kuhakikisha nakwenda shule. Aliyekuwa anashughulikia suala langu
ni Dk Katabalo ambaye sasa ni marehemu. Huyu ndiyo chanzo cha
mafanikio yangu, nimeazimia kwamba nitatenga siku niende angalau
nikaione familia yake na Mungu atanisaidia kutekeleza hili.
Dk Katabalo alianza kufanya mipango ya kufuatilia shule tatu ambazo ni Buigiri ya Dodoma, Furaha ya Tabora na nyingine ilijulikana kwa jina la Iganga ya nchini Uganda. Waliojibu haraka maombi ya kunipokea ni shule ya Buigiri, hivyo mwaka 1968 nikawasili hapo nikisindikizwa na baba yangu.

Nilihitimu darasa la saba mwaka 1974 na katika darasa letu tulikuwa wanafunzi 10, wawili tukachaguliwa kujiujunga na Shule ya
Sekondari Mpwapwa.
Mpwapwa ni shule ya kawaida na ndani ya darasa letu, watano kati yetu tulikuwa ni wenye ulemavu wa kutoona. Mwaka 1978 tulihitimu kidato
cha nne name nikachaguliwa kwenda sekondari Mirambo Tabora.
Swali: Ikoje safari yako katika upande wa elimu ya juu?
Jibu: Mwaka 1982 nilijiunga na
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nikisomea fani ya elimu na kuhitimu mwaka
1985. Nikarudi tena hapohapo kufanya shahada ya uzamili katika sayansi
ya jamii, kabla ya kwenda Chuo kikuu cha Manchester, Uingereza kuchukua
masomo ya udaktari wa falsafa mwaka
1994.
1994.
Darasa letu nchini Uingereza lilikuwa na wanafunzi
20 na mimi nikiwa mlemavu pekee. Hata hivyo tuliofanikiwa kupata
shahada tulikuwa watatu, wengine tukawaacha.
Swali: Ili uwe profesa ni lazima
pamoja na mambo mengineyo utoe machapisho ndani na nje ya nchi, unaweza
kutaja baadhi ya machapisho uliyoandika?
Jibu: Machapisho niliyotoa ni
pamoja na Teacher Education for Special Education in Tanzania lililotoka
katika jarida la Journal of Issues and Practice in Education - JIPE
(2004); Technologies
Deployed by Visually Impaired and Blind people in Tanzania to access Information katika jarida la Journal of Issues and Practice in
Education – JIPE (2006)
Deployed by Visually Impaired and Blind people in Tanzania to access Information katika jarida la Journal of Issues and Practice in
Education – JIPE (2006)
Mengine ni Models in staffing Special Education in
Tanzania jarida la Huria Journal, Vol.VI (2006); Advocacy Groups and Advocacy Activities in the education of the Visually Impaired and
Blind People in Tanzania, jarida la Journal of Issues and Practice in Education – JIPE (2006).
Machapisho mengine ni Counselling at the Workplace in Tanzania: What
can distance Education do? (Jarida la Huria Journal, Vol. 13); Partnerships and Collaborations in Educational Services for Visually Impaired and Blind People in Tanzania jarida la Tanzania
Journal of Special Education – TJSE (2014).

Post a Comment