Rais Kikwete ameahirisha kulihutubia taifa kupitia "Wazee wa Dar" ambapo sasa ataongea nao Jumatatu wiki ijayo(Disemba 22, 2014). Ikulu imethibitisha na kusema muda utatangazwa.
Rais kikwete jana tarehe 19 alitarajiwa kulihutubia taifa kupitia wazee wa
mkoa wa Dar es salaam katika mkutano wake ambao ulikuwa ufanyike katika
ukumbi wa Hotel ya Blue Pearl,Ubungo jijini Dar es salaam.
Katika mkutano wake huo Rais Kikwete alitazamia kuzungumzia
mustakabali wa nchi sambamba na kuweka wazi juu ya sakata la
utekelezaji wa maazimio nane likiwamo la Bunge la kuwawajibisha viongozi
waliotajwa katika sakata la uchotwaji wa fedha bilioni 360 katika
akaunti ya Tegeta Escrow Pamoja na mambo mengine.
Katika maazimio nane ya bunge yaliyopendekezwa yalitaka viongozi
waliotajwa katika ripoti hiyo kwa tuhuma za uchotwaji wa fedha
kuchukuliwa hatua za kinidhamu na hata wanapo bainika kufilisiwa mali
zao na kushitakiwa katika vyombo husika kwa kuonekana kulihujumu taifa
katika sakata hilo la uchotwaji wa fedha akaunti ya Escrow.
Rais pia alipanga kuzungumzia juu ya Sekta ya Elimu pamoja na agizo
lake la ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari nchini,Upigaji kura za
maoni kuhusu katiba Mpya utakao fanyika Aprili 30 pamoja na daftari la
wapiga kura.
Hata hivyo Katika Hotuba hiyo Rais aliazimia kuelezea uchaguzi wa
serikali za Mitaa ulivyo fanyika ambao ulionekana kukumbwa na dosari
kadhaa katika vituo vya kupigia kura katika sehemu mbali mbali za nchi
ulipo kuwa ukifanyika uchaguzi huo ambao uliweza kugharimu maisha ya
watu .
إرسال تعليق