SHAMSA AANGUA KILIO UWANJANI

MSANII wa filamu Bongo, Shamsa Ford  hivi karibuni alijikuta akiangua kilio uwanjani baada ya timu yake anayoishabikia ya Yanga kufungwa mabao mawili 
Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Taifa ambapo kulikuwa na mechi ya Nani Mtani Jembe 2 iliyozichezesha timu za Simba na Yanga ambapo Shamsa alijikuta akilia kama mtoto baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0.
“Unajua mimi ni Yanga damdam kufungwa imeniuma sana na nilishindwa kabisa kujizuia machozi, ukweli Yanga wanatukosea sana wao hawajui tu kwamba sisi mashabiki zao tunaumia,” alisema Shamsa.

Post a Comment

Previous Post Next Post