
Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Kenya ameikosoa vikali Marekani na
kusema kwamba sheria ya kupamabana na ugaidi ya nchini Kenya ni bora
zaidi kuliko ile ya Marekani.
Matamshi ya kiongozi huyo wa Kenya yametolewa baada ya makundi ya
upinzani nchini Kenya, baadhi ya nchi na mashirika ya kutetea haki za
binadamu ya ndani na ya kigeni kuikosoa sheria hiyo iliyotiwa saini siku
ya Ijumaa na Rais Uhuru Kenyatta.
Jennifer Rene "Jen" Psaki Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa
Marekani ameikosoa vikali sheria hiyo na kusema kuwa, Washington
imeingiwa na wasiwasi mkubwa kutokana na kuwepo mbinyo zaidi wa uhuru wa
raia kwenye sheria hiyo.
Kiongozi huyo wa Kenya ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa,
Marekani haipasi kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo, kwani sheria
iliyopitishwa ya kupambana na ugaidi ni bora kuliko ile ya Marekani.
Miongoni mwa vipengee vinavyopigiwa kelele ni sheria ya kuongezwa muda
wa kushikiliwa watuhumiwa wa ugaidi kutoka siku 90 za awali hadi karibu
mwaka mmoja.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
Chanzo: kiswahili.irib.ir
إرسال تعليق