SIMBA YASHINDA KESI DHIDI YA ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA, KULIPWA MAMILIONI

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeiagiza Etoile du Sahel kulipa kitita cha dola 300,000 (zaidi ya milioni 500) pamoja na faini.


Fifa imeitaka klabu hiyo ya Sousse nchini Tunisia kuhakikisha inalipa fedha hizo ndani ya mwezi mmoja pamoja na faini ya dola 28,000.

Hatua hiyo imefikia baada ya Simba kushinda kesi iliyotokana na Simba kushitaki kwa Fifa baada ya Etoile kushindwa kulipa fedha za malipo ya kumnunua Emmanuel Okwi (pichani juu).

Post a Comment

أحدث أقدم