Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akifuangua kikao cha Kamati
ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando.
Na.Aron Msigwa –MAELEZO.
Jiji la Dar es salaam linaangalia upya utaratibu wa kuwaondoa ombaomba
na wafanyabiashara ndogondogo(wamachinga) katika maeneo yasiyoruhusiwa
katika jiji la Dar es salaam kufuatia sheria na hatuazinazochukuliwa
ikiwemo kuwarudisha ombaomba hao katika mikoa wanayotoka kutokuzaa
matunda na kuwa endelevu kufuatia wengi wao kurudi katika maeneo ya
awali kila wanapoondolewa.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said
Mecki Sadiki wakati akifuangua kikao cha wajumbe wa Kamati ya Ushauri
ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) kilichofanyika leo jijini Dar es salaam
kujadili masuala mbalimbali ya mendeleo katika jiji la Dar es salaam.
Amesema kuwa kuendelea kuwepo kwa wafanyabiashara hao
katika maeneo yasiyo rasmi ni moja ya changamoto inayolikabili jiji la
Dar es salaam kutokana na biashara wanazozifanya kuchangia kuzuia maeneo
ya barabara ya waenda kwa miguu, kusababisha uchafuzi wa
mazingira,kusabisha msongamano wa magari kwa baadhi yao kuweka
bidhaa barabarani.
Amesema kutokana na hali hiyo baadhi ya wafanyabiashara
walio na biashara rasmi ambao hulipa kodi za Serikali wamekuwa
wakilamikia hali ya ukwepaji wa kodi inayofanywa na wafanyabiashara
hao.
Bw. Sadiki amesema mpango wa mkoa wa sasa ni kuendelea
kuwatumia wafanyabiashara hao kama fursa ya mtaji wa rasilimali watu
ambayo itatumika kama chanzo cha mapato katika kuleta maendeleo ya mkoa.
Amesema watendaji na viongozi wa halmashauri za mkoa wa
Dar es salaam wanalojukumu la kuweka mazingira mazuri ya kufanya
shughuli zao na kuwatumia katika shughuli za uzalishaji kwa utaratibu
mzuri utakaowekwa ili waendelee kunufaika na shughuli wanazofanya.
Akizungumzia kuhusu uboreshaji wa huduma za jamii
zikiwemo za Maji, Elimu na Afya katika jiji la Dar es salaam amesema
kuwa Serikali inaendelea kuzijengea uwezo shule kwa kuongeza majengo ya
madarasa, maabara na kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaofaulu elimu ya
msingi wanapata fursa ya kuendelea na masomo ya Sekondari.
Kuhusu huduma za afya amesema kuwa mkoa unaendelea na
maandalizi ya ujenzi wa jengo la ghorofa nane, eneo la Magomeni katika
manispaa ya Ilala litakalotumika kutolea huduma ya Afya ya Mama na Mtoto
na kuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 500.
“ Sasa tuko kwenye maandalizi ya ujenzi wa jengo maalum
la kutolea huduma ya Afya ya Mama na Mtoto katika jiji la Dar es salaam
litakalogharimu zaidi ya shilingi bilioni ishirini na moja, tayari
benki ya Tanzania Investment Bank imeshakubali kutoa mkopo kwa ajili ya
jengo hilo” Amesisitiza.
Aidha, katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam ametoa ufafanuzi kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika
nchi nzima Desemba 14 mwaka huu na kueleza kuwa baadhi ya maeneo ya
jiji la Dar es salaam ambayo uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo vurugu, uchaguzi huo utarudiwa ndani ya siku
saba.
Ameeleza kuwa katika mkoa wa Dar es salaam uchaguzi huo
ulitarajiwa kufanyika kwenye mitaa 561 lakini kutokana na changamoto
mbalimbali ulifanyika kwenye mitaa 491 na kuahirishwa kwenye kata 70.
Amelitaka jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa linaimarisha
ulinzi na usalama wakati wa marudio ya uchaguzi huo unaotarajiwa
kufanyika ndani ya siku 7 katika mitaa yote ambayo uchaguzi uliahirishwa
.
إرسال تعليق