Bagamoyo. Siku moja baada kuibuliwa pendekezo na Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuongeza mishahara watumishi wake,
Mkurugenzi wa Masoko wa TPDC, Joyce Kisamo amesema fedha hizo
hazijaombwa kwa ajili ya wafanyakazi wote na ametetea viwango hivyo kuwa
vipo chini ya hali halisi ndani ya sekta ya gesi na mafuta nchini.
Akifafanua pendekezo hilo katika warsha ya siku
mbili iliyoandaliwa na shirika hilo jana na kuhusisha watumishi wa
Serikali na vyombo vya habari, Kisamo alisema mishahara hiyo imeombwa
kwa ajili ya watumishi maalumu watakaosimamia mradi wa bomba la gesi
kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Alisema watumishi hao watakuwa wakifanya kazi
katika mazingira magumu ya kushinda porini kwa zaidi ya siku 28 na
kwamba uamuzi wa TPDC kuomba kiwango hicho cha fedha uliangalia
ushindani wa malipo katika soko.
Alisema kuna wakati walitangaza kazi kwa mameneja
wa mradi huo, wengi walijiunga na TPDC kutoka Songas, lakini baadaye
baadhi walirudi walikotoka kutokana na walichotakiwa kulipwa kuwa chini
ya matarajio.
“Watu wanashindwa kuelewa, fedha hizi hatujaomba
kwa ajili ya wafanyakazi wote ila ni kwa wale watakaohusika kuendesha na
kurekebisha mitambo ya usafirishaji gesi ambayo tumeigharimia kwa fedha
nyingi.
“Mtumishi huyu anafungiwa kwenye mitambo ili umeme
usikatike au usumbufu wowote usitokee, hivi Sh12 milioni kwa mwezi na
familia yake inamsubiria inatosha…mimi bado kwangu ni kidogo,” alisema
Kisamo.familia yake inamsubiria inatosha…mimi bado kwangu ni kidogo,”
alisema Kisamo.
Jana gazeti dada la The Citizen lilibainisha kuwa
TPDC kupitia mpango wa mradi wa kusafirsha gesi kutoka Mtwara hadi Dar
es Salaam imeomba kuwaongezea mishahara watumishi wake ambapo mtumishi
wa kima cha chini atatakiwa kulipwa Sh5.4 milioni na Ofisa Mkuu Mtendaji
kulipwa Sh36 milioni kwa mwezi. Pia, Watumishi hao katika pendekezo
hilo lililopelekwa Septemba kwa Baraza la Kutetea Walaji la Mamlaka ya
Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura-CCC), watapatiwa marupurupu manono
mbali na mishahara hiyo.
Watumishi wa kati wa shirika hilo, nyaraka hiyo
inapendekeza walipwe kati ya Sh12.6 milioni hadi Sh28 milioni kiasi cha
kuwafanya wafanane na maofisa Watendaji wa juu wa kampuni wanaolipwa
vizuri nchini.
Hata hivyo, Baraza la Kutetea Walaji la Mamlaka ya
Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura-CC) limeliita pendekezo hilo la
mishahara kuwa ni la “kusadikika” na “lisilo na uhalisia”.
Huku akionyesha kusikitishwa na kupingwa pendekezo
hilo, Kisamo alisema kiwango hicho kitakachotolewa kwa watumishi hao
maalumu ni kidogo sana na wala hakifafanishwi na kile wanacholipwa
baadhi ya watalaamu wengine katika kampuni nyingine zilizopo ndani sekta
hiyo nchini.
Aliongeza; “sisi tumeangalia industry (tasnia) ya
ndani pekee na hiki kiwango tulichoomba kimeshushwa na hakifanani hata
kidogo na inayolipwa na Songas. Nimeongea na Ewura na kuwaleza kuwa
‘tungediscuss’ (tungejadili) kabla ya kupelekwa nje kwenye mitandao.”
Alisema kutokana na mashaka hayo wananchi wanaweza
wakalikataa ombi hilo na kusababisha kuwakosa watalaamu ambao
wangesimamia mitambo hiyo ya usafirishaji ambayo bila kusimamia na
kuhudumiwa mara kwa mara itaharibika mapema.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق