Maeneo
mengi ya jiji la Dar es salaam hii leo wamefanya uchaguzi wa Serikali
za Mtaa ambapo wananchi wengi waliojitokeza wamejitokeza kutumia haki
yao ya msingi ya kidemokrasia ya kupiga kura. Picha mbalimbali
zikionesha watu wakishiriki katika zoezi hilo licha ya kasoro chache
zilizojitokeza kwa baadhi ya maeneo ambapo baadhi ya maeneo wameahirisha
uchaguzi huo kutokana na kukosekan kwa karatasi za kupigia kura huku
baadhi ya maeneo majina ya wapiga kura yakiwa hayana nembo stahili ya
mgombea mfano mgombea wa Chadema akawekewa nembo ya CUF.
Mkazi wa Kipunguni B, Onesphory Mrina akipiga kura yake.
Baadhi
ya vituo kam ahiki amani ilitawala hapa ni Kipunguni B huko Moshi Bar
kata ya Kivule Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.
Wakazi wa Mazizini wakihakiki majina yao.
Wakazi wa mazizini Ukonga wakisubiri kuingia kupiga kura.
Mkazi wa Mazizini Ukonga, Gerald Mugumira akionesha kidole chake baada ya kupiga kura yake ya kuwachagua viongozi wao.
Wakazi wa Mtaa wa Kilimahewa Wilaya ya Temeke , wakipiga kura
Wakazi wa Kilimahewa huko Temeke wakisubiri kupiga kura.
إرسال تعليق