![IMG_6695](http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2014/12/IMG_6695.jpg)
Mgeni
rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali
Hassan Rajab akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa kujadili
utekelezaji wa makubaliano ya haki za binadamu nchini na maandalizi ya
ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za
binadamu duniani.
Wengine meza kuu ni Katibu
Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay,
Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika
Mashariki Filiberto Ceriani-Sebregondi na Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika maadhimisho ya siku ya
haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili
utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
Na Mwandishi wetu
KAMISHNA
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ali Hassan Rajab amesema
kwamba suala la haki za mashoga, ni suala tata kwa kuwa ni kinyume cha
maumbile na sheria.
Kauli
hiyo ameitoa siku ya Haki za binadamu katika mahojiano na waandishi wa
habari kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazokabili Tume yake katika
kuhakikisha haki za biandamu nchini.
“Sisi
tumeumbwa na katika maumbile yetu kila mmoja alipewa haki yake sasa
tukiitumia isivyokusudiwa basi tunavunja haki. Tukitumia tunavyokusudia
tutakuwa juu ya mstari, “ alisema kamishna huyo na kuongeza kuwa kama
kuna watu wanahisi kuwa vile ni haki ajue kwamba anakwenda kinyume na
maumbile na sheria.
Kamishina
huyo alisema ingawa watu hao wanajivisha joho la haki za binadamu
wakisema ni haki zao kuwa mashoga, hiyo si utamaduni.
Hata hivyo alisema kuwa matendo hayo ni sawa na watu kuumbwa na mdomo kwa ajili ya kula chakula lakini mtu akapeleka puani.
Alisema
hayo ni maoni yake na kwamba watu hao wanapaswa kuelewa kuwa maumbile
hayaruhusu na vyema wajue sheria ili waweze kuishi vizuri.
“Ingawa
pengine utahisi kwamba hiyo ni haki yako na unayeifanya unaona haina
madhara, baadaye itakuwa na madhara. Madhara yake ni kama UKIMWI na
magonjwa ya gono na mengine kwa sababu tu ya kwenda tofauti ya maumbile
yanayotakiwa kwenda,” alisema.
Alisema
pamoja na ukweli huo katika masuala ya haki za binadamu kuwa kuna
changamoto nyingi katika suala hilo la haki za binadamu na utawala bora.
Alisema juhudi zinatakiwa kuelekezwa kwa wananchi kwa sababu ya kuwepo kwa mila nyingi zinazonyima haki.
Akizungumzia
mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola, alisema kwamba watu 80
walikufa kati ya mwaka 2006 na 2010 na kwamba sasa wanauliza wahusika
sababu ya mauaji hayo.
Alisema ni kazi ya Tume kuhoji matukio,sababu au mazingira ya vifo.
Siku
ya haki ya binadamu iliyoanza kusherehekewa mwaka 1948 pia kwenye
miaka ya 1990 ilianzisha mfumo wa mapitio wa kipindi maalumu ya nchi
kuhusu mpango mkakati wa haki za binadamu.
Mfumo
huo wa mapitio katika kipindi maalumu katika kujitathmini na kujipima
katika utekelezaji wa haki za binadamu ndio unaangalia yapi ya
kutekeleza katika kuhakikisha haki za binadamu zinapatikana siku zote.
إرسال تعليق