
Utafiti
mkubwa wa kisayansi umeonyesha kuwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa
Ukimwi vya HIV, vinapungua makali yake na kushuka kwa uwezo wake wa
maambukizi kwa jinsi vinavyobadilika. Watafiti katika chuo kikuu cha
Oxford nchini Uingereza wamefanya ugunduzi huo walipowafanyia uchunguzi
mamia ya wanawake nchini Botswana. Kikosi hicho cha madaktari kimegundua
kuwa virusi vya HIV vilikuwa vikiingia katika hatua ya kuharibu
mabadiliko yake ili kuishi na kwa kufanya hivyo, virusi hivyo kwa sasa
vinabadilika taratibu zaidi na inavichukua muda mrefu zaidi kusababisha
ugonjwa wa UKIMWI kwa watu wenye kuishi na virusi hivyo. Wanasayansi hao
wamesema kupungua kwa makali ya virusi vya HIV kutaweza kusaidia
jitihada za kutokomeza virusi hivyo, japokuwa wameonya kuwa virusi hivyo
dhaifu bado ni hatari kwa afya ya binadamu.

Maambukizi ya virusi vya Ukimwi yameshuka kwa asilimia 38 tangu mwaka 2001 na idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi vimepungua kutoka zaidi ya milioni 2.3 mwaka 2005 hadi milioni 1.5 mwaka 2013.
Haya yakiwa maendeleo mazuri, bado idadi kubwa ya watu wapatao milioni 35 wanaishi na virusi vya Ukimwi. Kila siku zaidi ya watu 5,700 wanaambukizwa virusi vya Ukimwi, sawa na watu karibu 240 kila saa.

Ugonjwa huu ni janga kubwa la kijamii duniani.UKIWMI si tu unawanyang'anya mamilioni ya watoto maskini kabisa, upendo na ulinzi kutoka kwa wazazi wao, bali pia watoto wengiwanabakia kuhangaika peke yao, wengi wakiwa na jukumu la kuwalea wadogo zao, katika hali ya umaskini mkubwa, kubaguliwa na unyanyapaa unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya HIV. Watoto wengi wanatengwa na mara nyingi ndugu wa familia zao hawawezi kuwatunza.
Post a Comment