
Polisi
nchini Uturuki wamemkamata mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka
kumi na sita kwa tuhuma za kumtukana Rais Recep Tayyip Erdogan.
Kwa
mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, kijana huyo alipelekwa
mahabusu baada ya kumtuhumu Bwana Erdogan na chama chake tawala cha AK
kwa vitendo vya rushwa wakati wa mkutano wa hadhara katikati ya mji wa
Anatolia.Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu ametetea kukamatwa kwa mwanafunzi huyo akisema ofisi ya rais lazima iheshimiwe.
Kumtukana mkuu wa nchi ni makosa kwa mujibu wa sheria za Uturuki na mwanafunzi huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka minne jela endapo atapatikana na kosa.(BBC)
Post a Comment