![](http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Kura--December15-2014.jpg)
Wananchi wakiwa katika wamepanga foleni kwenda kupiga kura jana
Tukio la kukuta majina yao yameshatumika kupiga kura lilijitokeza zaidi katika Kata ya Ngarenaro majira ya kuanzia asubuhi hadi mchana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM na mchumi, Wilaya ya Arusha, Emmanuel Sinyangwe, alisema katika uchaguzi huo kumekuwa na mapungufu kadhaa kama vile kuruhusu watu kupiga kura bila kuonyesha kitambulisho. Alisema hilo ni tatizo.
Mapema katika kituo cha kupigia kura Zainabu Msangi na Hadija Kadia walikamatwa baada ya kutiliwa mashaka kuwa hawakuwa wapiga kura halali wa eneo hilo. Diwani wa kata hiyo, Isaya Doita (Chadema), ndiye aliyewakamata na kuwafikisha kituo kidogo cha polisi ambako walishikiliwa.
Akizungumza ndani ya Kituo cha Polisi Ngarenaro, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngarenaro, Ephreim Maiky, alisema baada ya kuwahoji wapiga kura hao na kupata mashaka aliamuru kuitwa kwa balozi wa eneo hilo kwa lengo la kuwatambua.
Zainabu katika majibu yake kwa msimamizi wa uchaguzi alidai kuwa yeye mzaliwa wa Kata ya Daraja Mbili lakini ameolewa mtaa wa Kambi ya Fisi uliopo Kata ya Ngarenaro na ndiyo sababu amekuja kupiga kura.
Aidha alisema Hadija ni mdogo wake amekuja kumsaidia uzazi nyumbani kwake. Kwa upande wake alipohojiwa Hadija alidai kuwa Zainab ni mdogo wake majibu ambayo yalionyesha wasiwasi.
Lakini kukamatwa kwa wapiga kura hao kulipokelewa kwa hisia tofauti na Sinyangwe ambaye alimshutumu diwani huyo kwa kufanya kazi isiyo yake na kudai amefanya kosa kuwapiga makofi, wakati ni wapiga kura halali.
Diwani Doita, alisema watuhumiwa hao aliwakamata kituo cha Shule ya Msingi Unit ya mchepuo wa lugha ya Kiingereza wakiwa wanne na wawili kati yao walikubali kutumwa na CCM na kuamua kukimbia ila hao wawili ‘walikomaa’ na kufikishwa polisi.
Alidai kuwa CCM wamecheza mchezo mchafu wa kutuma watu kupiga kura wakati siyo majina yao na pia wengine wanaingia ndani wanakuta majina yao yamepigwa kura wakati hawajapiga kura.
Hata hivyo, upande wa CCM waliokuwepo eneo hilo akiwemo Sinyangwe, alidai balozi wa eneo hilo amekwenda kusimamia kura kwenye moja ya kituo, lakini baada ya saa moja kupita walirudi tena na kudai balozi huyo amekwenda kusimamia ubarikio wa mtoto wake hatakuja tena na askari walisimamia msimamo bila balozi halisi hawataruhusiwa kupiga kura.
Polisi waliwaachia baada ya balozi wa eneo husika kushindwa kufika lakini hawakuruhusiwa kupiga kura.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment