CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeanza
kukusanya saini za wananchi wa King’ongo kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo
tayari wameandika kuyapinga kwa msimamizi wa uchaguzi wilaya ya
Kinondoni.
Tayari hadi kufikia jana saini zaidi
ya 200 zimekusanywa .
Ukusanyaji wa saini hizo ambazo
zinakusanywa ndani ya mtaa huo ambao upo kata ya Saranga unafanyika kutokana na
msimamizi wa uchaguzi wa mtaa huo, Rebecca Rioga kudaiwa kutangaza mshindi
kinyume na utaratibu.
CUF ambao walishiriki katika kivuli
cha ukawa wamesema pamoja na CCM kutangazwa mshindi, hawakuwa wameshinda kwani
kilichotokea ni msimamizi kukiuka utaratibu katika uthibitishaji wa
kura.
Ushindi wa CCM ulitangazwa saa tano
usiku chini ya usimamizi wa Polisi kutoka kituo cha Mbezi.
Awali mawakala wa CUf wakati wa
kuhesabu kura pamoja na ushindi waliokuwa nao waliona kuna idadi kubwa ya kura
zinazozidi ambazo pia zina mfumo mmoja wa mkunjo na kupigiwa mgombea
wenyekiti wa CCM . Kura hizo zilipata
32.
Mzozo wa matokeo ulianzia hapo kwani
msimamizi alishindwa kueleza zilipotokea kura 32.
Jumla ya kura zote zilizopigwa
zilikuwa 930 kati ya watu 1,364 waliojiandikisha kupiga kura, lakini idadi ya
kura zote za wagombea uenyekiti ni 956 zikiwa ni kura 32 zaidi hasa baada ya
kura 6 .
Katika barua ya kupinga matokeo kwa
msimamizi wa uchaguzi halmashauri pamoja na kueleza bayana nini kilitokea
katika uchaguzi huo pia wamesema kwamba mgombea Demetreus Mapesi wa CCM
alitumia nafasi ya yeye kuwajua wasimamisi kutengeneza hila ya ushindi
mwishoni.
Mapesi ni mwenyekiti wa Shule ya
Msingi King’ongo ambacho kilikuwa kituo cha kupigia kura na wasimamizi pia
wanatoka shule hiyo hiyo.
Katika kura kituo A waliopiga kura
walikuwa 485 na kituo B waliopiga kura walikuwa 445 na kufanya jumla kuwa
930.Wagombea uenyekiti CUF Abubakari Nyamguma kituo A alipata kura 253 na
kituo B 224 ambapo mgombea wa CCM Demetreus Mapesi kituo A alipata kura 232 na
kituo B 247 .
Ukijumlisha kura walizopata wagombea
zinakuwa 956 na kuwa na ongezeko la kura 32.
mwisho
إرسال تعليق