Watoto Dar hatarini

  Dampo lawaathiri, wahara damu, wakohoa Huokota mipira ya kiume, bomba za sindano.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
Utupaji taka hovyo katika maeneo ya makazi ya watu umeelezwa kuhatarisha afya za watu, hasa watoto wadogo, jambo ambalo linahitaji hatua za haraka kuchukuliwa na serikali. Mfano ni dampo lisilo rasmi katika kata ya Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam, ambalo limeanza kuathiri watoto kutokana na kuzuka kwa magonjwa ya kuharisha damu na kukohoa.
Uchunguzi wa NIPASHE Jumamosi katika eneo hilo umeshuhudia taka hizo zikiwa ni zile  zinazozalishwa kutoka viwandani, majumbani na hospitalini. Hadi sasa walioathirika na taka hizo ni watoto ambao wameugua ugonjwa wa kuharisha damu na wengine kikohozi kisichoisha kutokana na kuvuta hewa chafu. 
 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

أحدث أقدم