
Dar es Salaam. Watanzania kila kona walikuwa wakifuatilia
mwenendo wa Bunge, licha ya kukatika kwa umeme kutokana na hitilafu
zilizokuwa zikijitokeza.
Zifuatazo ni siku tisa muhimu za sakata la
uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, lililoibuliwa
bungeni na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kabla ya Kamati ya
PAC inayoongozwa na Kabwe Zitto kulifanyia kazi, baada ya taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Novemba 22
Moto wa kashfa ya ufisadi katika akaunti ya Tegeta
Escrow unaoendelea kuwaka bungeni, sasa unaonekana kugeuka gharika
inayoweza kuwakumba vigogo wengi zaidi na kuiweka Serikali ya Rais
Jakaya Kikwete katika hali ngumu.
Kashfa hiyo ya uchotaji wa Sh306 bilioni za
akaunti ya Escrow, inahofiwa kuwakumba vigogo zaidi ya 50 ndani ya
Serikali wakiwamo mawaziri, makatibu wakuu, wabunge, majaji na wakuu wa
taasisi za Serikali.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa kutokana na
kuwapo kwa idadi kubwa ya mawaziri na watendaji wa Serikali na Mahakama,
hali hiyo inatishia anguko la Serikali.
Novemba 23
Hali ilikuwa tete.
Ndiyo neno ambalo unaweza kulizungumza kuhusu kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mji wa Dodoma ulikuwa umejaa pilikapilika zikiambatana na mikutano iliyokuwa ikijadili kashfa hiyo.
Kamati ya Uongozi wa Bunge, Kamati ya Uongozi wa
Wabunge wa CCM na Baraza la Mawaziri, kwa nyakati tofauti walikaa
kujadili ripoti ya Escrow ambayo ilijadiliwa na Bunge Jumatano na
Alhamisi wiki iliyopita.
Kikao cha wabunge wa CCM kilifanyika kujadili
suala hilo. Wabunge walionekana kila kona ya Viwanja vya Bunge jana
wakijadiliana katika vikundi kuhusu sakata la escrow, huku wengine
wakitaka hata miswada yote iliyobaki isijadiliwe ili kutoa nafasi
kuichambua kwa kina kashfa hiyo.
- Soma Zaidi Mwananchi
- Soma Zaidi Mwananchi
Post a Comment