Waandamanaji Misri
Serikali
ya Misri imesema watu kumi na wanane akiwemo Polisi mmoja wameuawa
wakati wa maandamano yaliyofanyika nchini humo wakati wakiadhimisha
miaka minne tangu kuangushwa utawala wa Hosni Mubarak.
Vifo hivyo
vimetokea mjini Alexandria na cairo,Serikali ilipiga marufuku
kuadhimisha kumbukumbu hizo hali iliyosabbaisha vurugu kati ya
Waandamanaji na Polisi.
Zaidi ya watu 400 pia wanashikiliwa
kutokana vurugu hizo.Hata hivyo serikali ilipiga marufuku tukio hilo
linalodaiwa kuwa ni la kumbukumbu ya maandamano 2011.
Maandamano
hayo ya mwaka 2011 nchini Misri yalikuwa yakiratibiwa na makundi ya
Waislam wenye msimamo mkali ambapo vikosi vya usalama vilishindwa
kuwadhibiti waandamanaji hao







إرسال تعليق