Kijana akiwa na nondo makalioni baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.
MWANAUME
mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni
alionja joto ya jiwe kwa kuchomwa nondo katika kalio lake la kushoto
baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu wilayani Tarime, Amani
limedokezwa.Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na wahusika, mwanaume huyo anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtu anayetajwa kwa jina moja la Marwa kwa muda mrefu, kitu kilichomfanya kujisahau na wakati mwingine kufanya vitendo vinavyoashiria mapenzi waziwazi akiwa na mwanamke huyo wa mwenzake.
“Wapambe wakampelekea habari jamaa ambaye alichukizwa sana na jambo hilo hasa kwa vile alikuwa akimgharamia sana mke wake. Baada ya kushauriana na watu wake wa karibu wakakubaliana kuandaa mtego ambao hata hivyo ili ufanikiwe, ilibidi mkewe ahusishwe.
“Wanadai mke alitishwa, kama hatakubali kufanikisha jambo hilo basi atauawa, maana atatoa siri nje, akakubali na kufanikisha zoezi hilo. Alipokutwa, jamaa aliamriwa kulala kifudifudi kisha nondo iliyochongwa ikachomwa upande wa juu wa kalio usawa wa kiuno, ukatokezea upande wa pili. Ni tukio la kusikitisha sana,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Mara, lakini hakuweza kupatikana kwa simu yake ya mkononi, ila ofisa mmoja mkubwa, aliyekataa kunukuliwa kwa vile siyo msemaji, alisema hana habari na tukio hilo.
“Taarifa tulizonazo ni kutoka kule Bunda, ambako hata hivyo ni tukio linalomhusu mwanamke, ambaye ameingiziwa chuma sehemu zake za siri na mwanaume kwa sababu ya wivu wa kimapenzi.”
Amani lilimsaka Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Rorya, Lazaro Benedict Mambosasa, ambaye alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema hata yeye anasikiasikia, ingawa halijamfikia rasmi ofisini kwake. Aliahidi kufuatilia zaidi suala hilo.

إرسال تعليق