Ahadi za JK zaitesa CCM, Nape asema Rais ametekeleza, wasomi , wanasiasa wasema utekelezaji ni mdogo

Nape asema Rais ametekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi zake, wasomi , wanasiasa wasema  utekelezaji ni mdogo
Dar es Salaam. Ahadi zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa wananchi katika mikutano mbalimbali nchini  wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, huenda zikawa mwiba kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, kutokana na nyingi kutokutekelezwa au kuwa katika hatua za mwanzo.
Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, kwa nyakati tofauti alitoa ahadi kusaidia kuwakwamua wananchi kutoka kwenye dimbwi la umaskini, maradhi na kuboresha upatikanaji wa elimu nchini. Ahadi hizo zilitarajiwa kukamilika kabla hajatoka madarakani.
Ikiwa imebaki takriban miezi 10 ya uongozi wa kipindi cha pili cha awamu ya nne kufikia ukomo, muda unakwenda haraka na utekelezaji wa ahadi hizo unasuasua jambo linalotia shaka iwapo kila ahadi itatekelezwa kwa wakati.
Kushindwa kutekeleza ahadi hizo ambazo zimo katika kitabu cha ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za urais 2010, kilichondaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kunaiweka Serikali ya CCM katika wakati mgumu hasa pale itakaporudi kwa wananchi kutoa ahadi nyingine kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ujao.
Nape
Alipoulizwa kuhusu ahadi hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema Rais Kikwete ametekeleza ahadi zaidi ya inavyoahidi ilani ya CCM.
 “Ukitaka kumtendea haki Rais Kikwete katika utekelezaji wa ahadi zake, lazima uangalie kitabu chote cha ahadi harafu upate ushahidi wa viongozi wawakilishi au kuzunguka kwenye maeneo zilizokotolewa ahadi hizo,” alisema na kuongeza;
“Kwa ufupi tu, Rais huyu amefanikiwa kutekeleza ahadi nyingi ambazo ziko kwenye ilani na zile alizotoa papo kwa papo.”
Hata hivyo Nape alimwahidi mwandishi wa gazeti hili kutoa ufafanuzi wa ahadi zilizotekelezwa na Rais kwa kipindi chote alichokaa madarakani wiki ijayo.
Turuka
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Florens Turuka alisema ofisi yake kwa sasa iko kwenye uchambuzi na uandaaji wa kitabu kitakachoeleza utekelezaji wake
- Mwananchi

Post a Comment

Previous Post Next Post