Nape asema Rais ametekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi zake, wasomi , wanasiasa wasema utekelezaji ni mdogo
Dar es Salaam. Ahadi zilizotolewa
na Rais Jakaya Kikwete kwa wananchi katika mikutano mbalimbali nchini
wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, huenda zikawa mwiba kwa
CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, kutokana na
nyingi kutokutekelezwa au kuwa katika hatua za mwanzo.
Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM
Taifa, kwa nyakati tofauti alitoa ahadi kusaidia kuwakwamua wananchi
kutoka kwenye dimbwi la umaskini, maradhi na kuboresha upatikanaji wa
elimu nchini. Ahadi hizo zilitarajiwa kukamilika kabla hajatoka
madarakani.
Ikiwa imebaki takriban miezi 10 ya uongozi wa
kipindi cha pili cha awamu ya nne kufikia ukomo, muda unakwenda haraka
na utekelezaji wa ahadi hizo unasuasua jambo linalotia shaka iwapo kila
ahadi itatekelezwa kwa wakati.
Kushindwa kutekeleza ahadi hizo ambazo zimo katika
kitabu cha ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Jakaya
Kikwete wakati wa kampeni za urais 2010, kilichondaliwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, kunaiweka Serikali ya CCM katika wakati mgumu hasa pale
itakaporudi kwa wananchi kutoa ahadi nyingine kwenye kampeni za uchaguzi
mkuu ujao.
Nape
Alipoulizwa kuhusu ahadi hizo, Katibu wa Itikadi
na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema Rais Kikwete ametekeleza ahadi
zaidi ya inavyoahidi ilani ya CCM.
“Ukitaka kumtendea haki Rais Kikwete katika
utekelezaji wa ahadi zake, lazima uangalie kitabu chote cha ahadi harafu
upate ushahidi wa viongozi wawakilishi au kuzunguka kwenye maeneo
zilizokotolewa ahadi hizo,” alisema na kuongeza;
“Kwa ufupi tu, Rais huyu amefanikiwa kutekeleza ahadi nyingi ambazo ziko kwenye ilani na zile alizotoa papo kwa papo.”
Hata hivyo Nape alimwahidi mwandishi wa gazeti
hili kutoa ufafanuzi wa ahadi zilizotekelezwa na Rais kwa kipindi chote
alichokaa madarakani wiki ijayo.
Turuka
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Florens
Turuka alisema ofisi yake kwa sasa iko kwenye uchambuzi na uandaaji wa
kitabu kitakachoeleza utekelezaji wake- Mwananchi
إرسال تعليق