Mbunge
wa jimbo la Manyoni Mashariki Mh. John Chiligati pamoja na Mbunge wa
jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji wakipungia mikono wakazi wa
Singida wakati wa mikutano ya chama cha Mapinduzi mkoani humo.
JIMBO LA MKALAMA.
Hili
kwa sasa linafananishwa na ‘mzoga’ kwa madai hadi sasa kuna dalili ya
watu 12 wanaonyesha dalili la kuliwania jimbo hilo ambalo zamani
lilikuwa likijulikana kwa jina la Iramba mashariki.
Mbunge
wa sasa Salome Mwambu wa CCM ambaye anamaliza kipindi chake cha kwanza
mwakani,anatarajiwa kutetea nafasi yake hiyo.Hata hivyo anatarajiwa
kupata upinzani mkubwa kutoka kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa sasa na
mbunge wa zamani wa jimbo la Iramba mashariki,Mgana Msindai.
Baadhi
ya watu wengine waliojitokeza ni pamoja na Alan Mkumbo wa TRA makao
makuu,Dc wa wilaya ya Nchemba,Francis Izack,Emmanule Mkumbo,mkandarasi
Nakei na Emmanuel Mbasha.Hii ni orodha fupi tu ya watu wanaoliwania
jimbo hilo linalopakana na mkoa wa Manyara.
Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi na Naibu Waziri wa Fedha Mwigullu Lameck Nchemba.
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI.
Jimbo
hili ambalo kwa sasa Naibu Waziri Wa Fedha Mwigullu Lameck
Nchemba,ndiye mbunge anayemaliza kipindi chake cha kwanza mwakani,
Inadaiwa jimbo hilo lina kawaida ya kuwakilishwa kipindi kimoja tu
(miaka 5) na wapiga kura wanabadilisha mwakilishi mwingine.
Kwa
sasa licha ya Mwigullu kuonyesha dalili ya kutetea nafasi yake hiyo na
pia kuna minong’ong’o kuwa atagombea nafasi ya urais, anakabiliana na
upinzani kutoka wabunge wa viti maalum wawili wa mkoa huu (CCM)
,wanatajwa kulimezea mate jimbo hilo.Pia yupo ndugu moja ametambulika
kwa jina moja, Nkurlu, Profesa Kitila Mkumbo ambaye kwa sasa hana chama
na Juma Kilimba aliyewahi kuwa mbunge kabla ya kuangushwa na Mwigullu.
JIMBO LA SINGIDA MAGHARIBI.
Jimbo
hili kwa sasa linashikiliwa na Mohammed Missanga wa CCM kwa vipindi
vitatu. Jimbo hili ambalo limemegwa sehemu na CHADEMA,ninawaniwa na
Missanga mwenyewe kwa lengo la kuweka rekodi ya kuliwakilisha kwa miaka
20 (vipindi vinne).
Pia
wapo wanaCCM ambao kwa sasa wanapiga jaramba la kumwangusha Missanga
ambao ni pamoja na Eliwaja Mtinda (mbunge viti maalum CHADEMA),wanatajwa
vile vile wakuu wawili wa wilaya akiwemo Khambako wa wilaya ya Kishampu
mkoa wa ShinyangaLissu Mahanju na daktari wa binadamu ambaye jina lake
halijaweza kupatikana mara moja.
Mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, John Paulo Lwanji.
JIMBO LA SINGIDA MJINI.
Jimbo hili ambalo makao makuu ya mkoa yalipo, kwa vipindi vitatu sasa linawakilishwa vema na Mohammed Gullam Dewji (44).
Hata
hivyo,Dewji inadaiwa anakabiliwa na upinzani wa karibu kutoka kwa mwana
CCM mwenzake katibu mwenezi CCM mkoa na mwalimu wa shule ya msingi,
Mussa .Pia mwandishi wa habari, Josephat Isango na ndugu yake na mbunge
wa jimbo la Singida mashariki kupitia CHADEMA,Tundu,Vicent Mughwai wote
wa CHADEMA,wapo kwenye maandalizi makali lengo likiwa ni kuing’oa CCM
katika jimbo la Singida mjini.
JIMBO LA MANYONI MASHARIKI.
Jimbo
hili kwa kindi kirefu,linashikiliwa na John Chiligati wa CCM.Anatajwa
mwanaCCM mmoja amabye ametambulika kwa jina moja la Mtuka,ameonyesha
kila dalili ya kumg’oa Chiligati.Pia yupo afisa mwanadamizi wa benki
moja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja,kuwa naye
analitaka kwa udi na uvumba jimbo hilo kupitia tiketi ya CHADEMA.
JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI.
John
Paulo Lwanji,ni mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM kwa vipindi vitatu
sasa.Lwanji ambaye ni mmoja wa watoto wa hayati mzee Lwanji ambaye
katika uhai wake aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo,anatajwa kuwa
ataitetea nafasi yake hiyo kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
mwakani.Inadaiwa anataka kuhakikisha ndoto yake ya jimbo hilo
kupandishwa hadhi na kuwa wilaya,inatimia.
Kwa
sasa bado hawajajulikana watu wengine wanaolitaka jimbo hilo lenye
hifadhi ya wanyama pori la Rungwa.Hata hivyo,uwezekano wa CHADEMA kuweka
mtu wake,ni asilimia mia moja kwa madai kwamba katika uchaguzi wa mwaka
2010,kilifanya vizuri katika nafasi hiyo ya ubunge.
إرسال تعليق