Amtoboa mwenzake na chupa, kisa anaendesha gari huku anasikiliza simu


Fundi makenika wa Lagos alitiwa mbaroni baada ya kumchoma  dereva mmoja kwa chupa iliyovunjika kwa dai kuwa hakuwa mwangalifu na alikuwa anaongea na simu huku akiendesha gari.
Makenika huyo Olajide Olaniran  inadaiwa alimchoma Julius Joseph katika maeneo ya Ijaiye .
Katika mabishano kabla ya kuchomwa na chupa hiyo, Joseph naye alimtuhumu Olaniran kwa uendesha kinyume cha sheria za usalama barabarani.
Imedaiwa kuwa katika mabishano hayo, Olaniran alimchoma Joseph na chupa iliyovunjika kisha  kukimbia na simu za Joseph na fedha zake kiasi cha Naira 5000.
Imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo baadae alikamatwa na polisi na  Joseph kukimbizwa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Lagos State University Teaching Hospital huko Ikeja kwa matibabu.
Olaniran amefunguliwa shitaka la kushambulia na kuiba na kesi yake itasikilizwa Januari 26 mwaka huu

Post a Comment

Previous Post Next Post