Wastaafu Mwenge kupewa maeneo

Dar es Salaam. Serikali kupitia mrajisi wa vyama vya ushirika, imekiwezesha Chama cha Ushirika cha Ujenzi wa Nyumba Mwenge (MHCS Ltd), kupata eneo la kiwanja chenye ukubwa wa ekari 800 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa wanachama na vitega uchumi vingine katika eneo la Kibiki, Chalinze Mkoa wa Pwani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi wa ushirika huo Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa bodi hiyo, Hillary Mdaki alisema tayari Serikali imewakabidhi eneo hilo na wanachama 378 pamoja na hati za umiliki wa viwanja hivyo.
Alisema eneo hilo limepatikana baada ya maombi ya ushirika huo kwa Serikali.
Awali waliomba Bagamoyo, lakini wakapatiwa Chalinze na kupitia mikopo ya benki, nyumba za wanachama zitajengwa.
“Lengo ni kuhakikisha wanachama ambao wengi ni wastaafu wa Serikali wananufaika na ushirika,” alisema Mdaki.
“Pia bodi ina jukumu la kuhakikisha mradi wa majengo pacha yatakayokuwa na ghorofa 32 unakamilika,” alisema.
Alibainisha kuwa majengo hayo pacha yatajengwa eneo la Afrika Sana, Mwenge ambalo walipewa na Rais wa Awamu ya Kwanza, Julius Nyerere mwaka 1971

Post a Comment

Previous Post Next Post